KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 8 September 2011

Shule Hii; Miaka 50 Baada Ya Uhuru


 Ndugu zangu,
Kuna mwenzetu baada ya kuona picha hiyo ya kwanza juzi,ameniandikia ujumbe kuniuliza kama mtoto huyo alikuwa annaingia darasani au nyumbani.Naam,alitaka kujua kama kweli hiyo ni shule baada ya miaka 50 ya uhuru.

Ufafanuzi wangu;
- Hiyo ni shule ya msingi katika Tanzania yetu ya leo.
- Huyo ni  mwanafunzi anayeingia darasani na mbele ni walimu wa shule wanaoingia darasani kufundisha.
- Hao ni wanafunzi darasani
- Hiyo ni nyumba ya Mwalimu Mkuu
- Na shule ina tundu moja la choo.
Ni miaka 50 baada ya Uhuru wetu. Tafakari.

Maggid Mjengwa
Iringa.

No comments:

Post a Comment