KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 11 September 2011

Mtoto Anusurika Kwenye Ajali Mbaya,Wazazi Wake Wote Wawili Wafarikii Dunia

Hili ni gari aina ya Mitubishi Pajero likiwa eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo mbaya juzi majira ya saa 11:30 jioni barabara kuu ya Singida Nzega kilomita 15 kutoka mjini singida na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi watatu akiwemo mtoto mdogo wa miaka miwili.
Mtoto Yohanes Josephat ( mwenye umri wa miaka miwili) akiwa wodi namba mbili pamoja na msamaria mwema akiuguza jicho baada ya kutokea kwa ajli hiyo, hata hivyo wazazi wote wawili wa mtoto huyo baba na mama walifariki dunia.Picha na Habari na Mdau Richard Mwaikenda

No comments:

Post a Comment