KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 11 September 2011

Mfuasi Wa CCM Amwagiwa Tindikali igunga

MFUASI wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana, ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kubandika mitaani mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM. Tesha alitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Sala leo kwa gharama za CCM Kumekuwepo na kushutumiana kati ya vyama vya CCM na CHADEMA kutokana na matukio kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea, hasa katika kipindi hiki cha Kampeni kuelekea uchaguzi mdogo wa Mbunge wa jimbo la Igunga, kufuatia kujiuzulu kwa mbunge wa zamani wa jimbo hilo Bw. Rostam Azizi Vyombo vya usalama na ulinzi vinatakiwa kuwa katika hali ya tahadhari na umakini mkubwa kwa muda wote wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo, ili kudhibiti vitendo kama hivyo vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani na utulivu katika kipindi hiki cha kampeni jimboni humo.Picha na Mpiga Picha Wetu

No comments:

Post a Comment