KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday 6 September 2011

Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Korosho Nchini.


Mheshimiwa, Anna Margaret Abdallah
---

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa, Anna Margaret Abdallah (Mb) kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Korosho.

Sambamba na uteuzi huo, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe kwa mujibu wa Sheria ya Tasnia ya Korosho na 18 ya mwaka 2009, Kifungu cha nne (4) amewateua Wajumbe wengine Nane ili kuiongoza Bodi hiyo itakayosaidia kupeleka mbele sekta ndogo ya zao la Korosho.

Wajumbe wa Bodi hiyo ni kama ifuatavyo: Bwana Twahir Nzallawahe, Mtaalam wa Agronomia kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika; Bwana Muzamii Karamagi, Mwakilishi wa Wabanguaji wakubwa wa korosho na Bibi Tumpale S. Magehema, akiwa Mjumbe kutoka kundi la Wabanguaji wadogo wa Korosho.

Wajumbe wengine ni Bwana Madanga Allon, Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU), Bwana Yusuph S. Namila, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba Newala Cooperative Union (TANECU) na Dkt. Peter Massawe, Mtaalam na Mtafiti wa zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Zao la korosho Kanda ya Kusini, ARI – Naliendele.

Aidha, Waziri Maghembe amewateua pia Mheshimiwa Jerome Bwanausi, Mbunge wa Lindi, Profesa Haji Semboja, Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Bwana Hemed Mkali, Mkulima wa Korosho Mkoa wa Pwani na Bwana Mudhihir Mohammed Mudhihir Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi. Uteuzi huo unaanza mara moja na utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika,

Dar es Salaam,

Simu: 2861319; 0769-239946; 0718-128653

No comments:

Post a Comment