KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 24 September 2011

Makamu wa Rais Dkt. Bilal ahudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa Zambia


Rais Mpya wa nchi ya Zambia Bw. Michael Chilufya Sata akila kiapo katika sherehe zilizofanyika jana mjini Lusaka Zambia mara baada ya kushinda na kumuangusha rais wa sasa wa nchi hiyo Mh. Rupia Banda ambaye tayari ameshakubali kushindwa katika uchaguzi huo ulikokuwa na upinzani mkubwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Rais Mstaafu wa Zambia,Mh. Ruphia Banda kwenye ofisi za Mahakama Kuu ya Zambia wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Michael Sata zilizofanyika jana mjini Lusaka Zambia.
(Picha na Amour Nassor VPO).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini,John Tendwa kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata mjini Lusaka jana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia), Mama Asha Bilal (kulia) na Rais mstaafu wa Zambia Ruphia Banda, wakimsikiliza Rais mpya wa Zambia Michael Sata alipokuwa akijitambulisha kwa viongozi wakuu wa Nchi mbalimbali waliohudhuria kwenye sherehe ya kuapishwa kwake iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia
katikati ni Mama Asha Bilal.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) na mkewe Mama Asha Bilal (wa pili kushoto), Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa (kushoto) na Rais wa kwanza wa Zambia,Dkt. Keneth Kaunda wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilala akisalimiana na Rais wa Malawi,Bingu wa Mutharika walipokutana kwenye Ofisi za Mahakama Kuu mjini Lusaka Zambia jana wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata

No comments:

Post a Comment