KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday 12 March 2012

CCM YAZINDUA KAMPENI ZAKE KWA KISHINDO ARUMERU MASHARIKI


. Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa akizindua kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki jana katika Uwanja wa Ngaresero. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akimnadi mgombea ubunge wa tiketi ya CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi huo kwenye Uwanja wa mpira wa Ngaresero jana.
Wananchi wa Arumeru Mashariki wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM.
Pamela Sioi Sumari akimnadi mumewe Sioi Sumari wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo za CCM. Pamela ni mtoto wa Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowassa.
Masanja wa Orijino Komedi akifanya manjonjo yake mbele ya umati, wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM
Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akizungumza.
Mratibu wa kampeni za CCM, jimbo la Arumeru Mashariki Mwigulu Nchemba akiongoza msafara wa waendesha pikipiki kuingia uwanjani kwenye uzinduzi kampeni za CCM. Kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Martine Shigella.

CCM: Mkutano Wa Uzinduzi


Ndg.Benjamin Mkapa akihutubia umati uliohudhuria uzinduzi wa CCM wa kampeni.

Kutokana na tatizo la mtandao tumeweka picha moja wakati tukihangaika kusubiri nyingine zinakuja hivi punde
 Katibu mkuu wa CCM Mukama


 Original Komedy wametumbuiza

Maanddalizi ya mkutano wa CCM, jimbo la Arumeru















Jana saa 10 jioni,na Mh.Benjamin Mkapa kwenye uwanja wa mpira Ngarasero

Bweni la Wasichana Lawaka Moto Chuo Kikuu Mkwawa


Kikosi cha Zimamoto na polisi wwakizima moto katika bweni la wasichana chuo cha Mkwawa mchana huu
Chumba cha wasichana katika chuo cha mkwawa kikiwaka moto Hivi ndivyo moto ulivyoteketeza vyumba viwili katika bweni la wasichana chuo cha Mkwawa
Hapa ndipo moto ulipoanzia katika bweni hilo
Chumba ambacho moto ulianza kuwaka kikiwa kimeteketea vibaya
Mali za wanafunzi zikiwa zimeteketea kwa moto
Polisi wakichukua maelezo kwa wahanga wa tukio hilo
Mmoja kati ya wahanga akiangua kilio baada ya kufika eneo la tukio na kukuta mali zake zimeteketea kwa moto




 










Moto mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza vyumba viwili vya bweni la wasichana maarufu kama Hall 6 vyumba Block W katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE) Iringa .

Mashuhuda wa tukio
walisema kuwa moto huo ulianza kuwaka katika chumba kimoja wapo chumba Block W muda wa saa 6 mchana na kuwa wakati huo baadhi ya wanafunzi walikuwa wamejipumzisha katika vyumba hivyo .

Sunday 11 March 2012

Chadema Waiteka Arumeru


BARABARA ZAFUNGWA, HELKOPTA YAPASUA ANGA,MBOWE ALIA WINGI WA POLISI, NASSARI AAHAIDI KUTATUA KERO ZA WANANCHI.
Waandishi Wetu, Arumeru
 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kiliuteka mji wa Usa River, wilayani Meru pale kilipozindua kwa kishindo kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.Shamrashamra za uzinduzi huo zilianza asubuhi na ilipotimu saa 7.40, helikopta yenye stika ya maneno CHADEMA, ilianza kuzunguka angani katika jimbo hilo, huku ikisambaza vipeperushi vinavyomnadi mgombea wa chama hicho, Joshua Nassari.

Mamia ya wapenzi na wanachama wa chama hicho walifurika katika Uwanja wa Shule ya Msingi, Leganga, Usa River kuazia saa saba mchana ambako uzinduzi wa kampeni ulifanyika zikiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mbowe na Nassari walifika kwenye Uwanja wa Leganga wakiwa kwenye helikopta saa 8.45 na kulakiwa na viongozi walioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe pamoja na wabunge kadhaa wa chama hicho.
Polisi pamoja na walinzi wa kikundi cha usalama cha Chadema, Red Brigade walipata wakati mgumu kuwadhibiti wafuasi waliokuwa wakitaka kusalimiana na viongozi hao walipowasili uwanjani hapo.
Hali hiyo pia iliwaathiri wapigapicha wa vyombo vya habari ambao walikwaruzana na polisi na walinzi wa Chadema walipokuwa katika harakati za kutekeleza majukumu yao.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa hakuhudhuria uzinduzi huo kutokana na kile kilichoelezwa na viongozi wa chama hicho kwamba yuko nchini Italia kwa safari ya kikazi.
Mbowe ambana Tendwa
Katika mkutano huo, Mbowe alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kutoa tamko juu ya CCM kukiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kutumia kiasi cha Sh220 milioni wakati wa mikutano miwili ya kupitisha mgombea wao wa ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Mbowe alisema Sheria ya Uchaguzi mdogo imeweka kiwango cha juu cha matumizi ya fedha ambazo zinapaswa kutumika zisizidi Sh80 milioni.

“Tunamuomba Tendwa atoe tamko juu ya hili, kwani mkutano wa kwanza wa CCM walikuwa na wajumbe 1,034 ambao kila mmoja alilipwa posho ya Sh50,000 na walitumia zaidi ya Sh100 milioni na mkutano wa pili ulikuwa na wajumbe1,044 ambao walitumia zaidi ya Sh120 milioni,” alisema Mbowe.

Alisema chama hicho, kilikuwa na wajumbe 888 na kilitumia kiasi cha Sh6.2 milioni pekee kutokana na usafiri na chakula kwa wajumbe.

Akizungumzia uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mbowe aliwataka wakazi wa jimbo hilo kutambua kuwa uchaguzi huo sio wa Meru pekee bali una sura ya kitaifa.

“Taifa zima linafuatilia Arumeru Mashariki kujua mnafanya nini, nawaomba sana mtuchagulie Joshua Nassari ili mtuongezee nguvu bungeni dhidi ya chama cha magamba kwani mbunge mmoja wa Chadema ni sawa na wabunge 30 wa CCM,” alisema Mbowe.

Kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mbowe alilalamika kwa kitendo cha kukataa vijana wenye umri unaofikia miaka 18 hadi 19 kutopiga kura sambamba na watu waliohamia Meru katika kipindi cha miezi 13 tangu kufanyika uchaguzi mkuu.

“Haki ya kupiga kura sio ya Tume ya Uchaguzi au Serikali ni haki ya kikatiba ya wananchi hivyo nimempigia simu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji mstaafu, Damian Lubuva lakini amesisitiza ambao watapiga kura ni wale waliojiandikisha mwaka 2009,”alisema Mbowe.

Mbowe pia alieleza kusikitishwa na uamuzi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) Saidi Mwema kuleta Meru magari zaidi ya 40 ya polisi, magari manne ya kumwaga maji ya kuwasha na shehena kubwa ya mabomu ya machozi.

“Mambo yote haya ya nini, tunaomba polisi mtuachie CCM tucheze nao na msitulaumu pale ambao mtasababisha vurugu,” alisema Mbowe.

Kauli ya Nassari
Kwa upande wake Nassari aliomba wakazi wa Meru wamtume kuwa mbunge ili awatetee ardhi yao, inayomilikiwa na wachache, asaidie kushughulikia tatizo la maji, ajira kwa vijana na masoko ya uhakika ya bidhaa mbalimbali, ikiwepo soko la kila wiki la Mbuguni

Nasari pia ambaye alimtambulisha mama yake mzazi na baba yake, jukwaani na kueleza walimsomesha hadi chuo kikuu kwa fedha za mbogamboga huku mama yake akipigwa na askari mgambo wa halmashauri.

Alisema hoja ya CCM kuwa asichaguliwe kwa kuwa hajaoa haina msingi.“Mbona wabunge wengine, Zitto Kabwe, John Mnyika na David Silinde ambaye tulikuwa naye chuo kikuu hawajaoa na wala hawana mpango wa kuoa mapema kama mimi, wamechaguliwa na wanafanya vizuri,” alisema Nassari.

Nassari(26) alieleza katika uchaguzi wa mwaka huu atahakikisha wanashirikiana na kulinda kura kwani kuna hofu ya kura zake kuibiwa kama ilivyotokea katika uchaguzi uliopita ambapo alichuana na marehemu Jeremiah Sumari.

Shamrashamra
Mbali na hamasa ya helikopta, uzinduzi huo pia ulishuhudia maandamano kutoka pande mbili za barabara kuu ya Moshi – Arusha, ambako kulikuwa na maandamano ya magari na mamia ya pikipiki zilizokuwa zimepambwa na bendera za Chadema na mabango ya picha za Nassari.Maandamano hayo yalisababisha kufungwa kwa muda kwa barabara hiyo na kukwaza usafiri kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Hali hiyo pia ilijitokeza wakati wa jioni baada ya kampeni kumalizika kwani misafara mirefu yenye magari na pikipiki ilisababisha msongamano katika barabara hiyo.
Kutoka upande wa Moshi maandamano ya pikipiki yaliongozwa na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, wakati kutoka mjini Arusha maandamano yaliongozwa na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema.
Muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo, aliingia farasi ambaye alikuwa amebeba mabango ya picha za Nassari na bendera za Chadema.
Viongozi wengine
Zitto aliwaomba wananchi wa Arumeru kuenzi msingi ulioasisiwa na wazee wao kwa kusimama kutetea haki dhidi ya uonevu akitaja tukio la mwaka 1951 walipochanga fedha na kumtuma Mzee Japhet Kirilo kwenda Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), kudai ardhi ya Meru iliyokuwa ikikaliwa na walowezi wa kikoloni.
“Meru mlimtuma Mzee Kirilo UN kudai ardhi yenu, sasa ni wakati wa kumtuma kijana wenu Nassari (Joshua) kuwatetea bungeni. Ubora wa Nassari hauko kwenye ujana wala elimu yake, bali chama chake cha Chadema anachotoka ambacho kimejipambanua kuwa mtetezi wa haki Tanzania,” alisema Zitto
 
Zitto aliwataka wana Arumeru.... Soma zaidi: http://www.mwananchi.co.tz

Mkutano Wa Uzinduzi CHADEMA






Wanakijiji,kumradhi tumechelewa kuweka picha hizi kutokana na tatizo la umeme hapa Arumeru.kutwa nzima kulikuwa mgawo, umerudi usiku na mitandao inaleta shida.Tutaendelea kujitahidi ili mpate picha mapema zaidi.