KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Friday 9 September 2011

CHADEMA WAZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE IGUNGA


Mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw Joseph Kashindye akihutubia wakazi wa mjini Igunga katika uwanja wa Sokoine jana jioni wakati wa uzinduzi rasmi wa mkampeni za chama hicho katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga ili kujaza nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mh. Rostam Aziz.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa akihutubia katika mkutano huo wakati wa zunduzi wa kampeni kwa chama chake.
Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa jimbo la Hai Mh. Freeman Mbowe akihutubia wakazi wa Igunga huku Joseph Kashindye mgombea ubunge wa jimbo hilo akisikiliza kwa makini.
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi akiwahutumia wakazi wa Igunga.
Mabango yalikuwa ni mengi lakini pia jeshi la polisi lilihakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha.
Kutoka kulia ni katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa, Joseph Kashindye mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga katikati na Mwenyekiti wa Chama hicho na mbunge wa jimbo la Hai wakielekea kwenye mkutano.
Wananchi wa Igunga wakielekea kwenye mkutano wa CHADEMA.
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akiwahutubia wananchi wa jimbo la Igunga jana jioni katikauzinduzi wa kampeni za ubunge jimboni humo.

No comments:

Post a Comment