KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday 31 July 2012

Magazeti Leo Jumanne




















Reactions::
Wabunge Wazidi Kuongezewa Marupurupu

MARUPURUPU ya wabunge ikiwamo mishahara imeongezwa kutoka Sh7.4 milioni kwa mwezi hadi takriban Sh11milioni kwa mwezi, hatua ambayo imeibua mjadala mwingine mzito miongoni mwao.

Tangu mwaka jana, wabunge wamekuwa katika vita ya kupokea au kutopokea posho ya vikao ambayo imekuwa ikikolezwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambaye alizikataa akisema mbunge anapokuwa kazini hahitaji kulipwa.

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba sasa vita kubwa ipo katika marupurupu mapya ambayo pamoja na kuchanganya na mshahara yanafikia Sh11milioni kwa mwezi.

Spika wa Bunge, Anne Makinda alipoulizwa jana alithibitisha kuhusu kuongezeka kwa malipo jumla ya wabunge kwa mwezi lakini akasema hafahamu kiwango halisi kilichoongezwa.

Makinda alisema nyongeza iliyopo siyo kwa wabunge tu, bali watumishi wote wa Serikali na ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), wakati wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2012/13.

“Hiyo nyongeza siyo tu kwa wabunge, bali ni kwa watumishi wa Serikali. Tena hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma). Sasa ukiniuliza kiasi gani hapo ndipo sielewei, ila najua nyongeza ipo,” alisema Spika.

Lakini, vyanzo kutoka ndani ya Bunge vilisema kwamba nyongeza hiyo ambayo tayari imeingia katika mshahara wa Julai ni Sh3.6milioni, hivyo kufanya jumla ya fedha anazochukua mbunge kufikia kiasi hicho cha Sh11milioni.
“Hiyo ni vita, kuna wabunge wana hasira kweli hawataki wananchi wajue kama marupurupu yameongezeka.

Wanaona wananchi wakijua itakuwa ni tatizo kubwa, watapigiwa kelele lakini nyongeza hiyo ipo. Tayari wengine wamechukua tangu Ijumaa,” kilisema chanzo kimoja kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya wabunge kutoka kundi la wanaopinga posho kwa wabunge wamepinga pia nyongeza hiyo wakitaka fedha hizo zielekezwe katika sekta nyingine za kijamii.

Marupuru ya sasa
Hadi mwezi uliopita, mbunge alikuwa akipokea Sh7.4milioni kwa mwezi ambazo kati ya hizo Sh2.5milioni ni kwa ajili ya mafuta, Sh2.3 mshahara, Sh170,000 kwa ajili ya mshahara wa dereva, 100,000 kwa ajili ya katibu wa mbunge na posho ya jimbo.

Hata hivyo, katika nyongeza hiyo ya sasa haijawekwa wazi kwamba kiasi gani ni kwa ajili ya mshahara, fedha za mafuta ya gari la mbunge, za dereva, katibu na za posho ya jimbo na tayari baadhi ya wabunge wameanza kufuatilia mchanganuo wa nyongeza hiyo.

Chanzo:
Dk. Ndungulile atetea kiti IAS

na Abdallah Khamis
MBUNGE wa Kigamboni, Dk Faustine Ndungulile (CCM) amechaguliwa kuwa mwakilishi wa Bara la Afrika kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Ukimwi (IAS) ambapo atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne.
Hiyo ni mara ya pili kwa Dk. Ndungulile kushika nafasi hiyo baada ya kipindi cha mwaka 2008 - 2012 kumalizika.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Dk. Ndungulile, ilieleza alichuana na wagombea wengine 13 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambazo ni Ethiopia, Nigeria, Afrika Kusini, Rwanda, Kenya, Morocco, Sudan na Misri.
Alisema majukumu ya taasisi hiyo yenye makao makuu yake Geneva, Uswisi ni pamoja na kuhamasisha njia bora na ya kisasa katika mapambano dhidi ya ukimwi, kutoa elimu na kujenga uwezo wa wataalamu wa ukimwi katika vita dhidi ya ugonjwa huo.
Mtikisiko  
 

 
Wanafunzi wa shule za Msingi za Temeke wakiingia kwenye ofisi za Manispaa ya Temeke kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana na kuwasababishia kukosa masomo.Picha na Elizabeth Edward
WALIMU WAGOMA KILA KONA, WANAFUNZI NAO WACHACHAMAA, SERIKALI YAONYA, YATISHIA KUWAFUTIA MISHAHARA
Waandishi Wetu
NCHI imetikiswa. Mgomo wa walimu ulioanza jana katika sehemu mbalimbali nchini, umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu huku kukiwa na taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida yaliyoambatana na mgomo huo usio na ukomo.

Katika sehemu mbalimbali nchini, walimu waliripotiwa kugoma kwa kutoingia madarasani na wengine walifika kazini na kusaini vitabu vya mahudhurio kisha kuondoka hali iliyosababisha wanafunzi kurandaranda ovyo katika sehemu za miji iliyo karibu na shule hizo.

Mjini Dodoma ,wabunge jana walimbana Naibu Spika, Job Ndugai wakitaka shughuli za Bunge zisitishwe ili kujadili mgomo wa walimu ambao umeanza rasmi jana nchi nzima, na kuziacha shule nyingi zikiwa na walimu wakuu na wakuu wa shule pekee.

Hata hivyo, Ndugai alisema Bunge lisingeweza kujadili suala hilo kwani tayari Serikali ilikuwa imelifikisha mahakamani baada ya kushindwa kuafikiana na walimu katika ngazi ya usuluhishi.Wakati hayo yakiendelea, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema Serikali itafuta mishahara kwa walimu walioitikia mwito Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa kushiriki mgomo ambao alisema siyo halali.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Kawambwa pia aliwaonya walimu ambao alisema wamekuwa wakiwabughudhi wenzao ambao waliamua kwenda kazini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akiwa Mjini Morogoro aliwaagiza wakuu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo kuandaa orodha ya majina ya walimu wasiofika kazini Julai 30 na waifikishe kwa maofisa elimu wa wilaya kabla ya saa 2:00 asubuhi ya Julai 31.

Waandishi wetu katika sehemu mbalimbali nchini pia waliripoti kwamba katika baadhi ya shule, wanafunzi waliruhusiwa kurejea nyumbani mapema kwa maelezo kwamba hakukuwa na masomo.Hali hiyo ilizua kizaazaa kwani katika baadhi ya mikoa wanafunzi walicharuka na kuitisha maandamano hadi katika ofisi za maofisa elimu wa wilaya, wakitaka Serikali iingilie kati mgomo huo ili waendelee kusoma.

Kadhalika, baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali walinukuliwa wakitoa matamko ya kuwasihi au kuwaamuru walimu warejee madarasani, kauli ambazo hata hivyo, hazikubadili uamuzi wa walimu hao.

Wanafunzi waandamana
Maandamano ya wanafunzi yaliripotiwa katika Mji wa Tunduma, Mbeya ambako polisi walitumia mabomu ya machozi kuwadhibiti wanafunzi.

Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi katika Wilaya ya Mbozi mkoani humo waliandamana wakidai haki ya kufundishwa. Hata hivyo, maandamano hayo yaliingiliwa na vibaka ambao baadaye walivunja ofisi za Halmashauri ya Mji wa Tunduma na kuiba mali kadhaa kisha kuchoma nyaraka zilizokuwemo.
Tukio hilo lilitokea asubuhi wakati wanafunzi wa shule 14 za msingi zilizopo katika halmashauri ya Tunduma walipojikusanya na kufanya maandamano hadi nyumbani kwa diwani na baada ya kumkosa walielekea kituo cha polisi na baadaye ofisi katika hizo.

Katika manispaa ya Temeke, Dar es Salaam zaidi ya wanafunzi 400 wa shule nne za msingi wameandamana hadi katika Ofisi ya Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo kupinga mgomo huo.
Wanafunzi wao ambao waliandamana walitoka katika Shule za Msingi Bwawani, Mbagala Kuu, Mtoni Kijichi na Maendeleo.

Wilayani Tarime, Mara wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi jana waliandamana hadi Ofisi ya Ofisa Elimu wa Wilaya hiyo na zile za CWT, wakidai haki yao za kupata elimu baada ya walimu kugoma kuingia madarasani na kisha kuwataka wanafunzi kurejea nyumbani.

Wanafunzi hao walisikika wakiimba na baadaye kuzungumza mbele ya Ofisa elimu wa Wilaya, Emmanuel Johnson kwamba kitendo cha walimu kugoma kufundisha kinawaathiri wao, hivyo waliitaka Serikali kuwalipa walimu madai yao ili waendelee na kuwafundisha.

“Watoto tunataka haki zetu, Watoto tunataka kupata elimu, watoto tunataka kusoma tunaomba walimu walipwe madai yao tuingie madarasani, watoto tusinyimwe haki yetu ya kupata elimu walimu wanapogoma waathirika ni sisi wanafunzi Serikali tatueni mgomo wa walimu,” walisema wanafunzi hao.
Johnson aliwatuliza wanafunzi hao na kuwaahidi kwamba atatatua tatizo hilo, hivyo kuwataka kurejea shuleni leo kuendelea na masomo.

Mkoani Pwani mgomo wa walimu ulisababisha maandamano yaliyowahusisha wanafunzi wa shule za msingi kadhaa katika Wilaya za Kisarawe, Mkuranga, Bagamoyo na Kibaha waliokuwa wakiishinikiza Serikali kusikiliza madai ya walimu ili wao waweze kupata haki yao ya kufundishwa.

CWT wanena
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Olouch alisema mgomo wa walimu umefanikiwa kwa asilimia 90 nchi nzima na kwamba walimu katika mikoa mbalimbali hawakwenda kazini ikiwa ni hatua ya kushinikiza kupewa haki yao.

“Tunawashukuru walimu kwa kuunga mkono azimio lao ambalo walilipigia kura la kufanyika kwa mgomo na kubaki nyumbani bila ya kwenda kazi hadi pale Serikali itakaposikiliza matatizo yao” alisema Oluoch na kuongeza:

“Mgomo huu ambao umeanza leo (jana) hautahusiana na Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika usiku wa kuamkia Agosti 26, mwaka huu.”
Oluoch alisema kikomo cha mgomo huo ni pale itakapotolewa taarifa na Rais wa CWT, Gratian Mukoba na si mtu mwingine yeyote wala Serikali.

“Walimu wanatakiwa kutambua kuwa mgomo huu utaendelea hadi pale Rais Mukoba atakapowatangazia kinachoendelea hivyo kwa hivi sasa waendelee na mgomo huu,” alisema Oluoch.

Serikali yang’aka
Akizungumzia mgomo huo Dk Kawambwa alisema: “Tutatumia sheria kwa kushikilia malipo ya mishahara kwa walimu wanaogoma na tutatumia pia sheria kuwaadhibu walimu wanaowabughudhi wenzao kwa kuwalazimisha wagome.”

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Kazi ya mwaka 2004 ambayo vyama vya wafanyakazi vinaitumia kufanikisha migomo, Kifungu cha 83(4) kinaeleza kwamba mfanyakazi hatapaswa kulipwa mshahara katika kipindi chote ambacho itatokea amegomea utoaji huduma kwa umma.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Dk Kawambwa alisema Kuwa Serikali itahakikisha kwamba inawalinda walimu wote ambao hawaungi mkono mgomo huo aliodai ni haramu kwa kuwa suala hilo kwa sasa linashughulikiwa mahakamani.

Katika hatua nyingine, Dk Kawambwa aliwaonya wazazi kuhakikisha kwamba watoto wao hawatumiwi na wagomaji kwa kuhimizwa kufanya maandamano na vurugu.
  Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu amewataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kujihusisha na hongo kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.

Wabunge wengine watatu gazeti la MWANANCHI limeshindwa kuwataja kwa kuwa hawakupatikana kuzungumzia tuhuma dhidi yao.

Katika orodha hiyo wamo wawili wa Viti Maalumu na mmoja wa jimbo na Lissu alidai kwamba wamekuwa wakishiriki vikao vya Kamati ya Nishati na Madini huku wakijua kuwa wana maslahi binafsi na wengine kutumia fursa hiyo kujinufaisha, “Kwa takriban juma moja sasa kumekuwa na mjadala mzito wa ufisadi hapa bungeni, sasa Kambi Rasmi ya Upinzani imejitathmini na kuona kwamba wabunge wake hasa walioko kwenye Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, John Mnyika, David Silinde na Mwanamrisho Abama hawahusiki,” alisema Lissu na kuendelea: “Ila uchunguzi wetu umefanikiwa kupata majina ya wabunge wanaohusika moja kwa moja na mgongano wa kimaslahi ambao tunaona tuwataje kwa maslahi ya umma.”

Lissu alikwenda mbali zaidi na kutaja tuhuma zinazowahusu wabunge hao akisema wawili ambao gazeti hili halikuwaja, wamejihusisha kufanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) hivyo wana mgongano wa kimaslahi.

Alisema Mwijage ana mgongano wa kimaslahi katika mchakato mzima wa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kampuni ya Puma Energy kwa kuwa yeye ni mtalaamu mwelekezi wa kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 50, “Nasir Abdalah na Mariam Kisangi; Hawa wanamiliki vituo vya mafuta. Sasa kwa namna yeyote ile kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini hawawezi kutenda haki katika mchakato wowote unaohusu suala la mafuta,” alisema na kuendelea; "....(jina limehifadhiwa) hana mgongano wa moja kwa moja wa maslahi, lakini kwa kadri tunavyofahamu, yeye ndiye aliyekuwa akiyafanyia kampeni ya kupata zabuni makampuni ya mafuta ya Oryx na Camel na ....(jina limehifadhiwa), suala lake ni complicated kidogo. Maslahi aliyonayo katika suala hilo ni kuwa ana uhusiano wa Kimapenzi na kigogo mmoja katika Wizara ya Nishati na Madini.”

“Hawa ndiyo wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambao sisi Kambi ya Upinzani tunawafahamu kuwa ndiyo waliojihusisha na mgongano wa kimaslahi. Tumewaangalia wabunge wetu wote watatu hawamo ila kama kuna mtu ana taarifa zinazowahusu, aseme na tutazifanyia kazi.”

Lissu alisema kitendo cha wabunge kujihusisha na mgongano wa kimaslahi na taasisi za umma ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na ni kinyume na maadili ya kibunge.

Katika hatua nyingine Lissu amemshauri Spika wa Bunge Anne Makinda kuzivunja pia kamati za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) akisema nazo zina madudu mengi, “Hili lisiishie tu kwa kuvunja Kamati ya Nishati na Madini, tunataka pia kamati za POAC na LAAC zivunjwe, uchunguzi ufanyike na wahusika waitwe kujitetea na hatimaye wenye hatia watajwe hadharani bungeni na majina yao yachapishwe kwenye magazeti ili haki itendeke,” alisema.

Alipoulizwa CHADEMA imefanya nini dhidi ya Mbunge wake, Zitto Kabwe kutajwa katika orodha hiyo, alijibu: “Nikiri kwamba sisi taarifa tunazo ila hatujamwita kumwuliza. Naomba ieleweke kwamba kama chama au Kambi Rasmi ya Upinzani hatuna maslahi na mbunge yeyote anayeonekana kujihusisha na masuala hayo.”
“Katika hili tunaomba uchunguzi ufanyike na matokeo yake yatangazwe ili tupate msingi wa tuhuma hizo na ninaahidi kwamba tutazifanyia kazi ipasavyo.”

MAJIBU YA WATUHUMIWA

Alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo, Kisangi alikiri kumiliki kituo cha mafuta lakini akasema sheria haimzuii mtu kama mambo yake anayafanya kwa uwazi, “Nimekuja bungeni nikitokea kwenye ualimu, nilikuwa nafundisha Shule ya Msingi ya Mianzini na biashara hii ni ya familia. Inaendeshwa kwa uwazi na mwanangu wa kwanza ndiye anayeisimamia. Kutokana na uwazi katika shughuli zangu, mwaka jana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilinipongeza. Mimi ni msafi na siko huko wanakofikiri wao (CHADEMA).”

Kwa upande wake, Mwijage alikanusha kuwa mtaalamu mwelekezi wa Kampuni ya Puma, badala yake akasema ni mtaalamu wa petroli anayefanya kazi ya kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nishati hiyo, "Siyo kweli, hawa wanadandia hoja. Mimi ni mtaalamu wa petroli ambaye mchango wangu kimsingi una faida kubwa bungeni na hata kwa jamii kwa ujumla. Sijafanya maamuzi yeyote ya kulihujumu taifa hili na hata kwenye Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini pekee, nilitoa mchango wa kurasa 10 kuhusu masuala hayo ya petroli,” alisema

Aliishauri kambi hiyo ya upinzani kuvuta subira, akieleza kuwa jambo lililoko bungeni linahusu ufisadi na uhujumu uchumi hivyo kauli zinazotolewa bila utafiti zinaweza kuvuruga mchakato mzima uliokwishaanzwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

Awali, Abdallah alipoulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki vituo vya mafuta hivyo kuwa na maslahi binafsi, alicheka na kuahidi kwamba angepiga simu baadaye, lakini hakufanya hivyo na alipopigiwa baadaye alikata simu. Hata hivyo, alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha kumiliki vituo vya mafuta.

Kamata kwa upande wake alisema: “Kuna kamati maalumu imepewa kazi ya kuchunguza mambo hayo, hivyo yote yanayoulizwa yatakuwa wazi na ukweli utajulikana tu. Nina maslahi au sina ukweli mtaujua, haraka ya nini?.

via gazeti la MWANANCHI

Monday 30 July 2012

Mke Wa Waziri Mkuu.Mama Tunu Pinda Azindua Mradi Wa Maji Hospital Ya Mawenzi
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akifunua pazia pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL anayemaliza muda wake Bw. Richard Wells kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wa maji katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi mjini Moshi, mradi huo ambao umefadhiliwa na kampuni ya bia ya Serengeti SBL umegharimu zaidi ya milioni 55 za kitanzania ulilenga kutoa suluhisho la muda mrefu katika matatizo sugu yayoikumba jamii hususani tatizo la uhaba wa maji safi kwa maendeleo ya maisha ya mtanzania, Kushoto katika picha ni Mkuu wa Wialaya ya Moshi Dk Msengi na yana uwezo wa kuhifadhi lita elfu 40.000 kwa wakati mmoja
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti B. Teddy Mapunda akitoa maelezo ya mradi huo kwa mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Bw. Richard. Wells anayemaliza muda wake.
Mkurugenzi mpya wa kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Bw. Steve Gannon akifungua bomba la maji mara baada ya mama Tunu Pinda anayeshuhudia tukio hilo kuzindua mradi huo kwenye hospitali ya Mkoa ya Mawenzi mjini Moshi leo, wapili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dk Msengi na kushoto ni Mkurugenzi wa Serengeti SBL anayemaliza muda wake Bw. Richard Wells.
Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akizungumza katika uzinduzi huo huku wakuu wa kampuni ya bia ya Serengeti wakimsikiliza kutoka kushoto ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa SBL Bw. Steve Gannon na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake Richard Wells.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo huku mgeni rasmiMama Tunu Pinda akifuatilia kwa makini.
Kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na uwajibikaji Bw. Malisa, Imani Lwinga Meneja Mawasiliano na Mtaalamu Masuala ya Fedha SBL Bw. John Collins.
Haya ndiyo Matenki ya maji katika mradi huo yataweza kuhifadhi lita elfu 40.000 za maji.
Mmama Tunu Pinda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Mawenzi kwa ajili ya kuzindua mradi wa maji kutoka kulia ni Mkurugenzi mpya wa SBL Bw. Steve Gannon, Mkurugenzi wa SBL anayemaliza muda wake B. Richard Wells na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama.
Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa SBL anayemaliza muda wake Bw. Richard Wells mara baada ya kuwasili kwenye Hospitali ya Mawenzi kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa maji, kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL na Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo Bw. Steve Gannon.
Kutoka kulia ni Mganga mkuu wa Mkoa wa Kiliamjaro Dk Mtumwa Mwako Steve Gannon, Richard Wells na Teddy Mapuinda wakimsubiri mgeni rasmi.

Mgeni rasmi mama Tunu Pinda akiwasili katika eneo la Tukio.
Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw. Ephraim Mafuru.
Baadhi ya wauguzi na wageni mbalimbali waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Teddy Mapunda akizungumza katika uzinduzi huo.
Bw. Richard Wells naye akatoa neno.
Wakuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti mstari wa mbele ni kutoka kulia ni Mkurugenzi mpya wa Kampuni ya Serengeti SBL Bw. Steve Gannon na Teddy Mapunda mstari wa nyuma kutoka kulia John Collins Mtaalam wa Fedha, Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji na Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko.
Mama Tunu Pinda akimsikiliza Bw. Richard WellsMkurugenzi wa SBL wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika hospitali ya Mawenzi leo.
Mkurugenzi wa Masoko SBL Bw. Ephraim Mafuru akizungumza katika mkutano huo.
Mama Tunu Pinda akipanda mti katika hospitali ya Mawenzi mara baada ya kuzindua mradi wa maji hospitalini hapo.
(picha zote kwa hisani ya Fullshangwe )

Wanafunzi wamlabua Mwalimu ambaye hakushiriki mgomo

Na Gideon Mwakanosya, Songea.

MWALIMU mmoja wa jinsia ya kike aliyefahamika kwa jina moja la Kahimba wa shule ya msingi ya Kambarage iliyopo Kata ya Msamala katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma amajeruhiwa vibaya kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili na kundi linalodaijwa kuwa ni la wanafunzi wa shule hiyo ambao wanadaiwa kuwa na hasira baada ya walimu wengi wa shule hiyo kutoonekana eneo la shule kufuatia mgomo wa chama cha Walimu (CWT).

Akizungumuza na waandishi wa habari hizi Mjini Songea mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kambarage Adolfina Ndunguru alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa ni udhalilishaji mkubwa kwa mwalimu kupigwa na wanafunzi.

Ndunguru alisema kuwa yeye pamoja na walimu wenzake hawakuweza kufika kwenye eneo la shule kwa kuwa wao ni walimu ambao wamekubaliana kugoma kutokana na Serikali kushindwa kutimiza ahadi yao wanayodai.

Alifafanunua kuwa inadaiwa kundi la wanafunzi lilipomuona mwalimu Kahimba kwenye eneo la shule hiyo lilimvamia na kuanza kumpiga mawe sehemu mbalimbali za mwili na baadaye alifanikiwa kukimbia.

Kwa upande wa baadhi ya walimu wa shule za msingi, Sekondari na Chuo cha Ualimu cha Songea kilichopo Manispaa ya Songea ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa mgomo utaendelea mpaka Serikali itakapo ridhia kuwalipa madai yao hasa ikizingatiwa kuwa wao wanafanyakazi katika mazingira magumu.

Waandishi wa habari walifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za Msingi na sekondari ambazo zilikuwa hazina walimu kabisa na kwamba wanafunzi wa shule hizo wakiwa wamezagaa mitaani huku wakiinung`unikia Serikali kwa kuto watendea haki walimu wao ambao alikuwa wakiwaandaa wanafunzi katika Mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi na sekondari.

Shule zilizotembelewa na waandishi wa habari ambazo hazikuwa na walimu kabisa ni Shule za Msingi za Matarawe, Mwembechai, Sabasaba, Mkombozi, Kawawa, Mfaranyaki, Majengo, Songea, Kambarage, Msamala na Majimaji na shule za sekondari za matarawe, Mfaranyaki, Shule ya wavulana Songea na Shule ya wasichana songea.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Majimaji Tamimu Ajali anayesoma darasa la tano ameiomba Serikali kuharakisha kutekeleza madai ya walimu wanayodai kwani bila kufanya hivyo kunauwezekano mkubwa wa kushuka kwa kiwango cha Elimu hasa ikizingatiwa kuwa wanafunzi wapo kwenye maandalizi ya kufanya mitihani.

Tamimu alisema kuwa ni vyema serikali ikatambua umuhimu wa mwalimu kwa kumuuongezea mshahara sawa na taaluma zingine muhimu kwa mfano. Wanajeshi, Madaktari,Wauguzi na wahudumu wa afya.

Afisa Elimu wa halmashauri ya Manispaa ya Songea Fulgensi Mponji amethibitisha kuwepo kwa mgomo huo wa walimu amabapo alisema Manispaa hiyo ina shule 72, Sekondari za Serikari 23, Shule za seskondari za binafsi 13 ambazo idadi kubwa ya walimu hawakuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.

Alisema kuwa tayari ameshawaagiza walimu wakuu wa shule za msingi na waratibu Elimu kata wote kukutananao katika shule ya msingi Mfaranyaki kwa lengo kuwakutanisha walimu ili kuzungumzia namna ya kutatua tatizo hilo.

Naye Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Ruvuma Luya Ng`onyani alisema kuwa mgomo huo ni halali na umezingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 80 (1) ambapo hatua ya kwanza CWT kwa niaba ya wanachama tayari imetekeleza kutangaza mgogoro wa siku 30 kwa kujaza fomu CMA No: 1.

---
habari via dj-sek.blogspot.com


Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakiandamana jana Jumatatu Julai 30, 2012, kupinga haki yao ya msingi ya kupata elimu kuvurugwa kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana. Wanafunzi hao waliandamana umbali wa kilomite 10 hadi ofisi za Afisa elimu wa manispaa hiyo na kueleza "kesi" yao ambapo wameitaka serikali kumalizana na walimu ili wao wasome.
Wanafunzi wa shule za Makuburi na Mabibo, wakiwa chini ya mwembe, jana asubuhi Jumatatu Julai 30. Walimu wengi hawakuingia madarasani kufundisha jana wakiitikia mwitoi kutoka chama cha walkimu nchini kilichowataka kutofanya kazi leo Jumatatu na kuendelea hadi madai yao kuhusu maslahi yatakaposhughulikiwa na serikali.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Makuburi, wakijisomea baada ya walimu shuleni hapo kugoma kufundisha jana Julai 30, 2012. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambaye hata hivyo alikataa kutaja jina lake, alisema walimu walifika lakini hawakufanya kazi wakiunga mkono agizo la rais wa chama cha walimu Gratian Mukoba, aliyewataka walimu wote kushiriki mgomo usio na kikomo kuanzai leo Jumatatu.
Afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Juliana Mlay (Kushoto) akitafakari nini cha kuwaambia "Wageni" wake, wanafunzi wa shule za msingi Kijichi na Bwawani za jijini walioandamana umbali wa kilomita 10 hadi ofisini hapo wakilaani kutosoma jana, kufuatia mgomo wa walimu ulioanza nchi nzima jana Julai 30, 2012.
Kiongozi wa wanafunzi walioandamana jana jijini Dar es Salaam, Christofa Msifuni Msuya wa darasa la saba, shule ya msingi Bwawani, akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye ofisi za Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 30, 2012.
Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi, zajijini Dar es Salaam, wakiamnadmana jana kupinga kile walichokiita kuvurfughwa kwa haki ya mtoto ya kupata elimu, na hii ni kufuatia mgomno wa walimu ulioanza jana nchi nzima. Wanafunzi hao waliandamana hadi urefu wa kilomita 10 kutoka shuleni kwao hadi ofisi ya Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, ziliko shule hizo, jirani na uwanja wa taifa ili kufikisha kilio chao.
Wanafunzi wakiwa wanaelekea ofisi ya Mkuu wa wilaya
Wanafunzi wa shule za msingi Vwawa wakiwa wanapiga vidumu huku wakielekea ofisi ya mkuu wa wilaya ni Baada ya walimu kugoma.
Moja ya wanafunzi wa shule ya msingi Meta baada ya kuona walimu hawajaingia darasani yeye alichukua jukumu la kuwafudnisha wenzake
Wanafanzi wa darasa la saba shule ya msingi Meta wakiendelea kupeana mazoezi ya masomo mbalimbali baada ya waalimu wao kugoma kuingia madarasani
Wanafuzi wapo makini kumsikiliza mwanafunzi mwenzao
Mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi muungano akiwa nje ya shule akichezea mchanga maana walimu wamegoma
Picha na Arithy via Mbeya Yetu blog
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mmoja, Salma Mtili akisahihisha daftari la mwanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo licha ya rais awa Chama cha Walimu Tanzaniza (CWT) kutangaza mgomo wa walimu nchi nzima.
Picha na Habari Mseto Blog

Wanafunzi wa shule ya msingi Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani katika Manispaa Singida (picha na Nathaniel Limu