KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 11 September 2011

Rais Jakaya Kikwete Ahudhuria Mkutano Uliojadili tatizo la Njaa na Ukame Linazozikabili Nchi za Pembe ya Afrika

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mwenyeji wakeRais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa siku moja uliojadili tatizo la njaa na ukame linazozikabili nchi za pembe ya Afrika uliofanyika katika kituo cha Umoja wa mataifa uliopo Gigiri, nje kidogo ya jiji la Nairobi,Kenya leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed jijini Nairobi kabla ya kuanza kwa mkutano uliojadili jinsi ya kukabiliana tatizo la njaa na ukame katika nchi za pembe ya Afrika.Katikati ni mwenyeji wa mkutano huo Rais Mwai Kibaki wa Kenya
Wakuu wa nchi walihudhuria mkutano wa ulijadili jinsi ya kukabiliana na tatizo la njaa na ukame katika nchi za pembe ya Afrika.kutoka kushoto ni Rais Salva Kiir wa Sudan ya Kusini,Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi,Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyopo Nairobi Bi.Sahle Work Zewle, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia na Makmu wa Rais wa Kenya Steven Kalonzo Musyoka.Picha na Freddy Maro-IKULU

No comments:

Post a Comment