KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 11 September 2011

Ajali Mbaya, Meli ya Abiria Yazama Zanzibar

Taarifa zilizo tufikia sasa zinasema  kwamba meli ambayo imesadikika kuondoka Unguja kuelekea Pemba  imezama, huku ikiwa imesheni abiria zaidi ya 500 wengi wao wakiwa ni wanafunzi ambao walikuwa wametoka rikizo ya Iddy, Mpaka sasa zaidi ya watu watano wamethibitika kuwa wamepoteza maisha, na wengine hawajapata msaada mpaka ilipo fika alfajiri.
 
Hata hivyo baadhi ya abiria walio kuwa pembezoni mwa upande wa meli amboo haijazama walikuwa wanafanya jitihada za kupiga simu kupata msaada bila mafanikio. meli hiyo pia inasemekana ilikua imeshena mizigo na kuzidiwa .
Hadi hivi sasa taarifa ambazo zimetufikia ni kwamba Zanzibar imekumbwa na msiba mkubwa. Kwa kifupi hali ni hiyo lakini kwa maelezo zaidi tutarifiana muda mfupi kutoka sasa kama hizi habari ni za ukweli na hali ikoje huko Visiwani jitihada za kuokoa watu bado kutokana na mawasiliano

No comments:

Post a Comment