KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday 13 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA JENGO LA MIHADHARA LA DUCE MILLIONI 158 ZACHANGWA KUSAIDIA UJENZI Inbox

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Jengo la Mihadhara na kuchangisha fedha za ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE jijini Dar es Salaam leo Septemba 13, 2011. Kusho ni mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDSM, Prof. Yunus Mgaya na (kulia) ni Mkuu wa Chuo hicho Kikuu Kishiriki cha DUCE, Prof. Salome Misana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuzindua Jiwe la Msingi la Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, uzinduzi uliambatana na uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, ambapo katika zoezi hilo la uchangishaji fedha Makamu alichangia Sh. Milioni 10, na kufanya jumla ya michango kufikia Sh. Milioni 158.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mchango wa sh. 60,000 uliotplewa na watoto wa Shule ya awali ya Duce kutoka kwa mtoto, Edna Mayungi, wakati wa zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya sekondari Chang’ombe lililofanyika wakati wa uzindu wa Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE leo Septemba 13 jijini Dar es Salaam. Katika zoezi hilo zilipatikana jumla ya Sh. Milioni 158 kwa njia ya ‘Cash’ Ahadi na Mnada. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Terezya Huvisa (kushoto) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, Prof. Salome Misana, baada ya kuzindua rasmi Jengo la Mihadhara la chuo hicho na kuendesha zoezi la uchangishaji fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo Septemba 13.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia picha yake iliyoandaliwa maalu kwa ajili ya kupigwa mnada katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari ya Chang’ombe, uliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki ch DUCE leo Septemba 13. Katika zoezi hilo zilipatikana Jumla ya Sh. Milioni 158 kwa njia ya Mnada, keshi na ahadi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya chumba cha mihadhara kilichopo katika jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, baada ya uzinduzi uliofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam leo Septemba 13.
 Watoto wa Shule ya awali ya DUCE, wakiimba ngonjela mbele ya mgeni rasmi, wakati wa uzinduzi huo leo.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais

No comments:

Post a Comment