KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday 16 August 2011

Walimu Shinyanga wakosa mishahara

 na Samwel Mwanga, Maswa

WALIMU wa shule za msingi na sekondari Wilaya ya Maswa, mkoani Shinyanga wamebainika kuishi maisha magumu na kushindwa kuhudhuria vipindi darasani kwa kukosa mishahara kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Hayo yamebainika jana katika kikao kilichoitishwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Kata ya Ipililo, baada ya viongozi wa chama hicho kuwaomba wanachama wao kusitisha tabia ya kukimbilia kukopa katika taasisi za fedha kama hakuna sababu za msingi.
Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa CWT Shinyanga, Kahema Musa, alisema chama chake kimegundua walimu wengi hawanufaiki na utitiri wa mikopo wanayopata kutoka katika taasisi lukuki za kifedha ambazo sasa zimewageuza kama shamba la bibi, kwa kuvuna riba kubwa kutokana na mikopo hiyo.
Hata hivyo alisema ni walimu wachache wanaoitumia vema mikopo hiyo kwa kufungua vitega uchumi na kujijengea nyumba za kuishi na familia zao huku wengine wakiitumia vibaya.
Naye mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa, Musa Maige, alisema hivi sasa kumeenea biashara ya kukopesha watumishi wa umma hususan walimu kwa kutumia mwanya wa mishahara midogo wanayopata isiyokidhi mahitaji yao.
Aidha, alisema kuwa CWT taifa imeamua kuanzisha benki ya walimu nchini itakayokuwa na tawi kila mkoa ili kutoa nafuu ya mikopo na kuwawezesha walimu kukopa kwa manufaa tofauti na ilivyo sasa licha kuwa riba yote itakayotozwa itarudi kuwanufaisha walimu hao.

No comments:

Post a Comment