KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 18 August 2011

TWENDE imedhamiria kutimiza malengo ya Milenia

Meneja Masoko wa TWENDE,Hamis Omary,akitoa maelezo kuhusiana na TWENDE,kulia Naomi Maro ,Mmoja wa wajasiriamali,katika mkutano na waandishi wa Habari,Hadees Dar-es- salaam,tarehe 18-8-2011
Meneja Mradi,Gloria Mongela,akitoa maelezo kuhusiana na TWENDE,kulia Naomi Maro ,Mmoja wa wajasiriamali,katika mkutano na waandishi wa Habari,Hadees Dar-es- salaam,tarehe 18-8-2011
Naomi Maro,mmoja kati ya wajasiriamali, kushoto ni meneja akitoa hoja kuhusu TWENDE,kushoto akiwa na Meneja Masoko wa TWENDE, katika  mkutano wa waandishi wa habari, ulofanyika Hadees ,tarehe 18-august-2011
 Naomi Maro,mmoja kati ya wajasiriamali, kulia, akiwa na Meneja Mradi na Meneja Masoko wa TWENDE wakijadiliana kuhusu TWENDE katika  mkutano wa waandishi na habari, ulofanyika Hadees ,tarehe 18-august-2011
----
Huu ni mwaka wa pili wa TWENDE ambao utafanyika tarehe 15, 16  na 17 Septemba mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar-es-salaam

Tunategemea mahudhurio zaidi mwaka huu,katika hafla ya TWENDE kama njia ya mawasiliano, kuendeleza na kuwahamasisha wanawake katika biashara zao kitaifa na kimataifa alisema Gloria Mongela meneja mradi wa TWENDE.

TWENDE imedhamiria kuchangia kutangaza malengo ya milenia ya 1,3,5 na 8, ambayo ni kuondoa umasikini na njaa, kutangaza haki na fursa  sawa kwa wote, na kuwahamasisha wanawake kwenye afya zao na kuwaendeleza uhusianao wa kudumu  kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

”Ningependa kusisitiza Uma kuhudhuria kwa kiasi kikubwa na kutumia fursa hii ya TWENDE kuuendeleza ujuzi wakijisaliamali kwa kuuonyesha bidhaa na huduma zao na pia kuhudhuria kwenye semina.Tunategemea ushirikiano mkubwa sio tu kwa marafiki na familia bali kwa wanawake wote wajasiliamali na jamii ya watanzania kwa ujumla”. Alisema Meneja Masoko wa TWENDE, Hamis Omary

Malengo ya TWENDE ni kuwakuza kibiashara wajasiriamali wanawake nchini hii itasaidia muongezeko wa wanawake  wuzalishaji na uwiano sawa kibiashara na kimasoko katika jamii iliyotawaliwa na Wanaume.

“ Tunaomba taasis za fedha ,maendeleo ya wanawake na watoo, na  mashirika yaliobobea katika maswala ya jinsia kushirikiana na  TWENDE ili kuweza kutimiza malengo ya Melenia namba 1,3,5 na 8, kwa kuwahamasisha wanawake wajasililiamari, kuhudhuria maonesho na pia kusambaza taarifa kwa uma kiujumla”,
aliongeza Mr.Omary.

Maonyesho ya TWENDE, ni bure kwa watu wote ,ambapo yatafunguliwa saa 4:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni, kuanzia tarehe 15-17 Septemba 2011.

 “Ninafurahia TWENDE,kwasababu inatoa nafasi ya wajasiliamali kukutana na kuwasiliana,na pia kupewa muunguzo mzuri katika biashara. Alsema Naomi Maro,Mmoja kati ya wanawake wajasiriamali,walioudhulia,mkutano wa Twende na waandishi wa habari.

Maonyesho hayo ya siku tatu yataambatana na semina ili kuweza kuwapa wajasiriamali wanawake mbinu za kuzishinda changamoto na kujiendeleza kibiashara.

TWENDE ,imedhaminiwa na Daily News, Habari Leo, Perfect Machinery, Ultimate Security, Global outdoor systems and 361 Degrees.

Ujumbe wa TWENDE 2011:
Mimi Mwanamke, Mimi mjasiriamali
Hatanisipowezeshwa nikiamua ninaweza
Mwanamke maendeleo

No comments:

Post a Comment