KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday 15 August 2011

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA



WAZIRI wa Habari, Vijana ,Utamadunina Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo(jana)na mpigakura wake kutoka Ruvuma Rajabu Said (kushoto).
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba wa pili kutoka (kushoto)na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma,Hawa Ghasia wa pili (kulia) wakizungumza katika viwanja vya Bunge leo(jana) mjini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalum, Zainab Vullu wa kwanza(kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum,Zarina Madabida wa kwanza (kulia) .
WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka wa pili kutoka (kushoto) akiwa na Naibu wake Goodluck Ole- Medeye wa pili kutoka (kulia) mara baada ya kuwasilisha hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ya wizarayake leo(jana) Bungeni mjini Dodoma.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba naMaendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka(katikati) akihojiwa na watayarishaji wa kipindi cha daladala (kushoto )ni Danny Kijo na( kulia) ni Christina Mbunda.

No comments:

Post a Comment