KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday 10 August 2011

ADHA YA UHABA WA MAFUTA BADO YAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM


Hii ndiyo adha ya mafuta iliyoendelea kulikumba jiji la Dar es salaam leo hasa muda wa asubuhi na mchana ambapo vituo kadhaa vilivyotii amri ya serikali ya kuwataka wamiliki wa vituo hivyo kuanza kuuza mafuta, watu walionekana wengi wakiwa na madumu kwenye foleni huku misururu mikubwa ya magari ikionekana, kama unavyoona mmoja wa watu akijaribu kuwapoza wenzake ambao walionekana kutoelewana wakati wakigombea kununua mafuta.
Hata hivyo baadhi ya vituo kandokando ya jiji la Dar es salaam navyo vimeanza kuuza mafuta jioni hii, ambapo katika kituo cha Kobil Urafiki maeneo ya Njiapanda ya Mabibo kilianza kuuza mafuta na kulikwa hakuna foleni, Hali hii imenipa nafuu na mimi niliyekuwa nahitaji sana mafuta manake nilikuwa sijui mustakabali wa kazi zangu kesho, kutokana na mafuta kupungua katika gari yangu.
Msururu wa wateja katika kituo cha Gapco kilichopo Posta mtaa wa Samora.
Msururu wa magari nao ukisubiri kujaza mafuta.

No comments:

Post a Comment