KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday 24 August 2011

Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Azungumza na Vijana wa Vikundi Mbalimbali Vya Ushirika Kutoka Pemba na Unguja, Wanaokwenda Nchini China kwa Ajili ya Masomo ya Ufugaji wa Samaki

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Vijana wa vikundi mbalimbali vya ushirika kutoka Pemba na Unguja, wanaokwenda nchini China kwa ajili ya masomo ya Ufugaji wa samaki ambao wanatarajiwa kuwa nchini huko kwa muda wa mwezi mmoja,mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
Hawa ni Vijana wa vikundi mbali mbali vya ushirika kutoka Pemba na Unguja, wanaokwenda nchini China kwa ajili ya masomo ya Ufugaji wa samaki ambao wanatarajiwa kuwa nchini huko kwa muda wa mwezi mmoja,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,alipozungumza nao Ikulu Mjini Zanzibar jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiagana na Vijana wa vikundi mbali mbali vya ushirika kutoka Pemba na Unguja, wanaokwenda nchini China kwa masomo ya Ufugaji wa samaki ambao wanatarajiwa kuondoka leo,na watakuwa nchini huko kwa muda wa mwezi mmoja, baada ya kuzungumza nao Ikulu Mjini Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa vikundi mbali mbali vya ushirika kutoka Pemba na Unguja, wanaokwenda nchini China kwa masomo ya Ufugaji wa samaki,kwa muda wa mwezi mmoja, Ikulu Mjini Zanzibar jana.Picha na Ramadhan Othman Ikulu-Zanzibar

No comments:

Post a Comment