KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 18 August 2011

Meya Wa Jiji La Dar es Salaam Atembelea Jengo La Machinga Complex; Aagiza Wanaomiliki Vibanda Kinyume Na Utaratibu Wanyang'anywe

Meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masabuli, akikagua moja ya vizimba ndani ya jengo la Machinga Complex alipotembelea jana asubuhi.
eya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masabuli, aizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea jengo la Machinga Complex jana asubuhi. Akifanya majumuisho ya ziara yake ya kukagua jeng hilo , Mstahiki Meya Masabuli,  aliagiza kuwa vyumba vyote vya biashara (vizimba) vilivyogawiwa kwa wafanyabiashara nna utaratibu virejeshwe kwa bodi mpya ya jengo hilo na shughuli ya ugawaji ifanyike upya.kodi ya zamani  kinyume Pia aliagiza kuwa vizimba 344 vilivyogawiwa na kwa wafanyabiashara katika jengo hilo ambavyo havitumiki vigawiwe upya.Aliagiza kutolewa kwa nyavu zilizotumika kwa ajiri ya kutengenisha vizimba ndani ya jengo hilo kwani vimewekwa pasipo kuzingatia umuhimu ya mahitaji kwa watumiaji. Vyavu hizo zilinunuliwa na kutengenezwa kwa thamani ya shilingi Bilioni 1.2
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masabuli,akizungumza na waandishi wa habari jana asubuji kwenye jengo la Machinga Complex jijini Dar es Salaam alipotembelea kukagua vizimba vya wafanyabiashara.
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masabuli akizungumza na akina mama wauza Batiki wanaofanya biashara hiyo pembeni ya jengo la Machinga Complex kutokana na kukosa nafasi ndani ya jengo hilo.Masaburi aliuagiza uongozi wa jengo hilo, kuwapatia nafasi akina mama hao haraka.
Waandishi wa habari wakiwa katika msafara na Meya wa ´jiji,  ndani ya Jengo la Machinga Complex jana asubuhi.Picha Zote na Mdau Victor Makinda

No comments:

Post a Comment