KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday 24 August 2011

Jeshi La Polisi Zanzibar Lakamata Magudia Ya Dagaa Yaliyojazwa Pembe Za Tembo

 HIVI ndivyo ilivyokuwa jinsi ilivyohifadhiwa
 Mkuu wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar SP Martin Lissu akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio bandarini Zanzibar wakati wa zoezi likiendelea.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar ACP. Muhud Mshihiri akizungumza na wakala wa kusafirisha mizingi na msimamizi wa mzingo huo, wakati wa zoezi la kuendelea kupekuwa magunia ya Dagaa ikiwa ndani yake mmeweka Pembe za Tembo, kulia Kamanda wa Polisi Marine Zanzibar SP Martin Lissu.  
 MMOJA ya Konteni lilokuwa likisubiri kusafirishwa na kago ya magunia ya Dagaa na kuchanganywa na Pembe za Tembo likiwa katika upekuzi baada ya kugundulika kuwa na Nyara za Serikali zikitaka kusafirishwa nje ya Nchi. 
 HIVI ndivyo ilivyokuwa kufunguwa kila gunia kutowa kisicho husika katika magunia ya Dagaa inayosemekana yakitokea Mwanza na kusafirishwa nje kupitia bandari ya Zanzibar.
 KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar. 
KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar.Picha Zote na Mdau Othman Maulid 
--
Na Mwandishi wa MAELEZO-Zanzibar
Polisi Visiwani Zanzibar wamekamata Shehena kubwa ya Pembe za ndovu katika Bandari ya Malindi Visiwani hapa.

Hii ni Shehena kubwa ya kwanza kukamatwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba ambapo Polisi walifanikiwa kuigundua baada ya taarifa za Kiintelijensia zilizofanyiwa kazi kitaalam.
Shehena hiyo ya Vipusa ilikuwa imepakiwa katika makontena mawili huku kukiwa na shehena ya samaki aina ya dagaa wa maji baridi.

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na Mamlaka husika, zinadai kuwa Shehena hiyo ya Pembe za Ndovu ilikuwa ikipelekwa nchini Malaysia.Hadi saa 1:00 usiku Polisi walikuwa wakiendelea na kazi ya upakuaji na upekuzi zaidi katika eneo la Bandari ambapo kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi Bandarini,Martin Lissu watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi.

Watu waliokamatwa ni pamoja na Wakala wa mizigo ambaye Polisi wamesema ni mapema mno kumtaja kwa sababu za kiupelelezi.

No comments:

Post a Comment