KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday 16 August 2011

Nyota Wa Mpira Wa Kikapu Marekani Achangia Ujenzi Wa Mabweni Monduli



1. Nyota wa mchezo wa kikapu nchini Marekani anayechezea timu ya Orlando Magic,Dwight Howard ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya D12 Foundation akiwa na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowassa pamoja na mkewe,Regina Lowassa mara nyota huyo alipotembelea shule ya sekondari ya wasichana ya Kipok iliyopo wilayani Monduli juzi na kutoa msaada wa kiasi cha fedha 90 milioni kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafuzi shuleni hapo.

2. Nyota huyo,Dwight Howard hapa akiwa na wanafunzi mbalimbali wa shule ya sekondari ya wasichana ya Kipok iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha mara alipotembelea shuleni hapo na kumwaga mamilioni ya fedha kusadia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi shuleni hapo.

3. Nyota huyo wa kikapu nchini Marekani anayechezea timu ya Orlando Magic akiwa na watu mbalimbali waliofika katika hafla ya kukabidhi hundi ya kiasi cha sh,90 milioni kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi shuleni hapo. Habari na picha na mdau wa Monduli.

No comments:

Post a Comment