KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday 25 July 2011

mwanamke Aolewa na Wanaume Wawili

Wanandoa Arcado Mlele (kushoto) na Paulo Sabuni (kulia)wakiwa na mke wao Veronica Salehe na watoto wao Fred na Wilson kwenye kijiji Ikondamoyo, wilayani Mpanda mkoani Rukwa, hivi karibuni.Picha na Peti Siyame
---
MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani hapa, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea....>>>>>

No comments:

Post a Comment