KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 28 July 2011

Naibu Waziri wa Utamaduni Kutoka Nchini China Amtembelea Waziri Mkuu Mizengo Pinda Mjini Dodoma

Waziri Mkuu,Mizengo Pinga, akiangalia  zawadi ya chombo cha kuwekea sukari alichopewa na  Naibu waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua (kulia) wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake  mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka nchini China, Zhao Shaohua, akiangalia zawadi ya picha ya pundamilia aliyopewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinga (kushoto)  wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake  mjini Dodoma leo. Zhao pamoja na ujumbe wake  wako  nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo, Emmanuel Nchimbi (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua (katikati) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mjini Dodoma leo Kulia ni Zhao Haisheng aliyeapambana na ujumbe huo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni, Anjela Ngovi, akimvalisha kanga Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua, wakati naibu waziri huyo alipotembelea mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuonana na viongozi wa Serikali  huku waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo, Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Prof. Helmasi Mwansoko (kulia) wakishuhudia .
 Naibu waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua, akiangalia ngoma ya kabila la kisukuma iliyokuwa inachezwa na kikundi cha ngoma cha Mwinamila cha mjini Dodoma baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili mjini Dodoma leo.Picha Zote na Anna Nkinda-MAELEZO

No comments:

Post a Comment