KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 2 July 2011

Maonesho Ya 35 Ya Biashara (Sabasaba),Fika Banda La Uhamiaji Upate Huduma Za Visa, Passport na CTA

Ni katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Monesho ya 35 YA Kimataifa yanayoendelea, ndani ya Jengo la Karume, palipo na Banda la Idara ya uhamiaji. Hapo utakutana na wahudumu wenye ujuzi, wanaoelekeza kwa ufasaha na kutoa huduma za Visa, Passport,  Visa ya muda mfupi, CTA na huduma nyinginezo muhimu. Ukifika Bandani hapo,utahudumiwa na kujifunza mengi yenye tija kwako na kwa Taifa Tanzania.
Msemaji Msaidizi Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan, akitoa maelekezo na kumpatia kipeperushi  mwananchi aliyefika katika Banda la Uhamiaji ndani ya jengo la Karume kwenye Viwanja vya  Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya 35 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Idara ya Uhamiaji wana machapisho na vipeperushi vingi ambavyo huwapatia wananchi wanaofika hapo wajisomee na kuelewa shughuli mbali mbali zinazofanywa na Idara hiyo nyeti.
Afisa wa Uhamiaji, Idara ya Uhamiaji, akimsikiliza kwa makini na kumuhudumia mwananchi aliyefika bandani hapo  kujaza fomu kwa ajiri ya kupata Passport.
Afisa Uhamiaji, Sophia Gunda, akimfafanulia jambo mwananchi aliyefika Banda la Idara ya Uhamiaji katika Maonesho ya 35 ya Kimataifa ya Biashara,  sabasaba.
Raia wa Kigeni akipata maelekezo sambamba na kuchukua vipeperushi katika Banda la Idara ya Uhamiaji katika  Maonesho ya 35 ya Kimataifa ya Bisahara, sabasaba. Picha zote na Victor Makinda.

No comments:

Post a Comment