KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 14 July 2011

Jul 14 Kampuni Ya Bia Tanzania TBL Yazindua Tenki la Maji lenye Ujazo wa lita 50,000


Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (wa pili  kulia), na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Pindi Chana (CCM), wakimtwisha ndoo ya maji Mama Mkazi wa Kijiji cha Lugarawa, Mary Luoga wakati wa uzinduzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita 50,000 lililojengwa kwa msaada wa Sh. milioni 15 za TBL katika kijiji hicho kilichopo wilayani Ludewa, Iringa.Makabidhiano ya tenki hilo yalifanyika hivi karibuni katika kijijini hapo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Lugarawa, Mathias Kihaule (kushoto), akiipongeza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kwa Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Dorris Malulu baada ya kukabidhiwa mradi wa Tenki la maji lenye ujazo wa lita za maji 50,000 lililojengwa kwa msaada wa sh. milioni 15 za TBL katika Kijiji cha Lugarawa, wilayani Ludewa, Iringa. Anayeshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika hivi karibuni katika Kijiji hicho, ni Mbunge wa Viti Maalum, Pindi Chana (CCM).
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Pindi Chana (CCM),wa pili kushoto, Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (wa tatu kushoto), Ofisa Tawala wa wa Wilaya ya Ludewa,Charles Keiya na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Lugarawa, Mathias Kihaule (kushoto) wakifurahia wakati TBL ilipokabidhi tenki la maji lenye ujazo wa lita 50,000 za maji katika Kijiji cha Lugarawa, wilayani Ludewa hivi karibuni.Ujenzi wa tenki hilo  umegharimu sh.milioni 15 zilizotolewa na TBL.
Doris Malulu wa TBL, akihutubutubia katika makabadhiano hayo.
Kwaya ya Umoja wa Wanawake wa CCM, wa Kata ya Lugarawa  wakitumbuiza katika hafla hyo
Wakazi wa Kata ya Lugarawa wakitumbuiza kwa ngoma wakati wa makabidhiano hayo

No comments:

Post a Comment