KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 7 July 2011

Nape Nnauye Akunwa na Ugunduzi Wa Gari Inayotumia Mionzi Ya Jua.Aishauri Serikali Kulinda Ajira Za Wazalendo

 Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Stadi(VETA),Emanueli Bukuku akiwa na gari aliyoiigundua ambayo haitumii mafuta. Gari hiyo inatumia mionzi ya Jua (Solara Power).Emanuel anasema alipata wazo hilo la kubadlishaja mfuo wa Gari kutoka kutumia mafuta na  kutumia Solar Power kutokana na bei kubwa ya Mafuta inayopanda kila kukicha.Anasema imemchukua miaka miwili toka kubuni mpaka kukamilisha matengenezo.Akielezea kuhusu Gari hiyo jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara(Sabasaba)Emanuel anasema kuwa Gari hiyo inauwezo wa  kutembea kilomita 100.Haina Injini.
 Mwalimu Emanuel Bukuku, akimwelekeza Katibu wa Itikadi na Uenezi  wa CCM Taifa, Nape Nnauye jinsi gari hiyo inavyozalisha  nguvu za jua na uwezo wa kutembea.Nape alitembelea Maonesho ya Kimataifa ya Biashara jana kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere na kufika katika Banda la VETA ndipo alipokutana na Mwalimu wa VETA na Mvumbuzi wa Gari isiyotumia Mafuta. Akizungumza baada ya Maelekezo hayo, Nape aliitaka serikali kuwekeza na kuwajali Wabunifu Wazalendo na kulinda ajira zao.Alisema kuwa kuna Vijana wenye uwezo mkubwa hapa nchini na  Serikali haina haja ya kuajiri watu kutoka mataifa mengine ikiwa tuna hazina kubwa ya ujuzi, wabunifu na Wachapakazi hapa nyumbani. Nape alimpongeza Emanuel Bukuku kwa Ugunduzi huo ambao alisema kuwa ukiendelezwa utakuwa na tija kubwa kwa Taifa
Sehemu ya Nyuma ya Gari hiyo ambayo hufungwa vifaa kwa ajili na kuzalisha Nguvu za jua.Picha na Mdau Victor Makinda

No comments:

Post a Comment