KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 16 July 2011

Gereza halina choo cha wafungwa tangu mwaka 1962 lilipojengwa



JIBU LA SWALI LA MBUNGE Viti Maalum

na Mwandishi wetu, Dodoma

GEREZA la Ngudu katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza halina choo tangu lilipojengwa 1962 na kwimba wafungwa wa gereza hilo wamekuwa wakijisaidia kwa kutumia ndoo, imeelezwa.
Hayo yalibainishwa jana na Mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere (CHADEMA) ambaye alisema kuwa hali katika gereza hilo ni mbaya na juhudi za makusudi zinahitajika.
Kutokana na hali hiyo, mbunge huyo alimtaka Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya, kufika katika eneo hilo na ikibidi akalale hapo kwa zaidi ya siku tatu katika eneo hilo ashuhudie namna wafungwa wa gereza hilo wanavyopata taabu.
“Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo lile hali ni mbaya kwani hawana choo tangu gereza hilo lilipojengwa na kwamba wanajisaidia kwa kutumia mitondoro (ndoo) lakini wanapokwenda kumwaga kinyesi hicho hawanawi mikono; namtaka waziri akakae pale kwa siku ili aweze kushuhudia hali hiyo,’’ alisema Nyerere.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Balozi Khamisi Kagasheki, alikiri gereza hilo kutokuwa na choo kwa muda mrefu lakini akisisitiza kuwa serikali inaliangalia kwa ukaribu tatizo hilo na ambapo wakati wowote watatatua tatizo hilo. Balozi Kaghasheki, alisema kuwa wafungwa hao wana haki kama walivyo raia wengine katika misingi ya haki za binadamu na hivyo akaahidi kuwa katika Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jambo hilo litazungumzwa.
Katika swali la msingi la mbunge wa Dole, Sylivester Mabumba (CCM), alitaka kujua ni wananchi wangapi wamepoteza maisha yao katika hospitali za serikali kutokana na mgao wa umeme katika kipindi cha 2009-2011.
Naibu Waziri wa Afya Dk Lucy Nkya alisema kuwa hakuna kifo chochote kilichoripotiwa kutoka mikoa yote ambacho kinatokana na mgao wa umeme nchini.
Waziri alisema kuwa hospitali nyingi zimechukua hatua za tahadhari za kuhakikisha kwamba umeme mbadala umekuwepo wakati wote kwa kutumia jenereta, umeme wa jua na aina nyingine za vyanzo salama vya mwanga kama karabai.

No comments:

Post a Comment