KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday 25 July 2011

Rais Jakaya Kikwete Ashiriki Mazishi Ya Mpigania Uhuru David Zimbihile

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo Nyumbani kwa mpigania uhuru na kada wa CCM,marehemu David Zimbihile(80) wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Muleba jana jioni.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu mzee David Zimbihile wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika Muleba Jana jioni.Mzee Zimbihile aliyewahi kuwa mbunge na kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama Cha Mapinduzi alizikwa kwa heshima zote kijijini mwake Muleba, mkoani Kagera
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la kada wa CCM na mpigania uhuru, mzee David Zimbihile wakati wa mazishi ya kada huyo mkongwe(80) yaliyofanyika Muleba,Mkoani Kagera jana jioni.
Mwenyekiti wa CCM ,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la mpigania uhuru na kada mkongwe wa CCM David Zimbihile wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Muleba,mkoani Kagera leo jioni.Marehemu Zimbihile alianza harakati za ukombozi wa mwafrika nchini Kongo(DRC) ambapo alifanya kazi kwa karibu na Marehemu Patrice Lumumba na baadaye kupitia vyama vya wafanyakazi alikutana na Marehemu Kwame Nkurumah na hatimaye alirejea nchini Tanzania kuendelea na harakati hizo.Picha na Freddy Maro-IKUL

No comments:

Post a Comment