KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday 25 July 2011

NAIBU SPIKA KATIKA MKUTANO WA 57 WA CPA UINGEREZA

Sunday, July 24, 2011



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati tendaji ya CPA Dunia mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo katika Mkutano wa CPAn Uingereza, . Mkutano 57 wa CPA umeanza jana Jijini London Uingereza na unatarajiwa Kufunguliwa rasmi Leo na Malkia wa Uingereza.
Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (kulia), Spika wa Namibia Mhe. Asser Kapete (katikati) na Mbunge kutoka Nigeria wakisikilza jambo kutoka kwa Desk Officer wa CPA tawi la Tanzania Said Yakubu mara baada ya kumaliza kikao cha kwanza cha kamati tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) kilichoanza jana Jijini London Uingereza.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, akifurahia jambo na Spika wa Malawi Mhe. Henry Chimuntu Banda mara baada ya kumaliza kikao cha kwanza cha kamati tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) kilichoanza jana Jijini London Uingereza.

Naibu Spika Mhe. Job Ndugai, akimkabidhi Katibu Mkuu wa CPA Dkt. William Shija zawadi ya Crystals yenye Picha ya Mlima Kilimanjaro
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Mhe. Mohamed Shafie Abdal, (Mb) Mwenyekiti Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) Dunia na waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Malaysia, zawadi Crystals ya picha ya Mlima Kilimanjaro mara baada ya kumalizika kikao cha kamati tendaji ya CPA ambapo Mhe. Ndugai anamaliza mda wake kama mwakilishi wa Nchi za Africa katika kamati hiyo. Mkutano 57 wa CPA umeanza jana Jijini London Uingereza na unatarajiwa Kufunguliwa rasmi Leo na Malkia wa Uingereza.

No comments:

Post a Comment