KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 7 July 2011

Rais Jakaya Kikwete na Wana CCM Washerekea Miaka 50 Ya Tanu Usiku Wa Kuamkia Leo

Rais Kikwete na Mzee Milinga wakishirikiana kubonyesha king'ora hicho
Baada ya burudani, Kikwete akiambatana na muasisi wa mstari wa mbele wa TANU kati ya wawili waliopo hai Costantine Milinga, kwenda kuliza king'ora ilipotimu saa sita kamili usiku wa kuamkia leo 
Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akiwa na Makamu wake, Pius Msekwa, Katibu Mkuu Wilson Mukama na mkewe Mama Kikwete baada ya kuwasili viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto ni, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Wapili kushoto Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita na kulia ni mlezi wa CCM mkoa huo, Abdulrahman Kinana.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais, Jakaya Kikwete alipowaili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam,katika sherehe ya mkesha wa kuzaliwa kwa TANU. Kulia ni Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abdulrahman Kinana.
Rais Kikwete akimsalimia Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM,  aliposalimia wana-CCM mbalimbali kabla ya kuondoka Lumumba
Rais Kikwete akimsalimiana wana CCM
Kisha akazikung'uta tumba
Nape akaona haitoshi, akapanda jukwaani na kucharaza gita zito la bass, kuwapa tafu Vijana jazz
Mama Salma Kikwete akamkubali kuwa kweli Nape ni mwanamuziki mahiri,akaenda kumtuza nteze kibao
Mamia ya watu upande wa lango la kuingia viwanja vya Mnazi Mmoja
Wana-CCM wakiserebuka nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba wakati wa mkesha huo wa kuzaliwa kwa TANU usiku wa kuamkia leo
Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete wakiondoka Lulumba, kwenda viwanja vya Mnazi Mmoja kuendelea na mkesha wa kuzaliwa TANU
Rais jakaya kikwete akaondoka akisindikizwa na Msekwa na Mukama na viongozi wengine
Nape akatumia fursa hiyo kuzungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kwa nyakati tofauti baada ya Mwenyekiti,Rais Kikwete kuondoka.Hapa anazungumza na watangazaji wa Uhuru FM.Picha na Mdau Bashir Nkromo

No comments:

Post a Comment