KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday, 10 October 2012



NMB YAKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI BUNGE

Wanafunzi  wa Shule ya Msingi Bunge wakiwa wameketi kwenye madawati  50 yenye thamani  ya shilingi milioni 5 waliyokabidhiwa na Benki ya NMB kama sehemu ya msaada kwa shule hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge iliyopo katika Manispaa ya Ilala, wakifurahia madawati 50 yaliyotolewa na benki ya NMB   kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la uhaba wa madawati shuleni hapo.
Meneja wa NMB Bank House Bw. Leon Ngowi (kulia) akimkabidhi dawati moja kati ya madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 yaliyotolewa na NMB Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge Bi. Hadija Telela. Wakishuhudia ni Meneja Huduma kwa Wateja wa NMB Bank House, Stephen Chavalla (Pili kushoto) na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Bunge Christina Wambura.

No comments:

Post a Comment