KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 13 October 2012


NSSF YAZINDUA OFISI MPYA WILAYANI ARUMERU


Mkurugenzi mtendaji wa NSSF Ramadhani Dau akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ofisi mpya ya mfuko huo katika eneo la Usa river Wilayani Arumeru mkoani Arusha leo
Aliyevalia suti nyeusi ni mkurugenzi mwendeshaji wa NSSF Cricentus Magori katikati ni mkurugenzi mkuu Ramadhani Dau wakiingia katika eneo la uzinduzi leo mjini Arumeru
Wadau mbalimbali,wafanyakazi na wanachama wa NSSF wakiwa ndani ya jengo hilo jipya ilikujionea namna ofisi zilivyokamilika tayari kwa huduma
…………………………………………………..
Ashura Mohamed – Arusha
Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF)  imezindua ofisi  mpya katika kata ya Usariver wilayani Arumeru ikiwa ni moja kati ya kuboresha huduma za wanachama wake katika wilaya hiyo ili  kuweza  kuwasogezea  huduma wananchi  karibu zaidi.
 Akizungumza katika  uzinduzi huo mkurugenzi mtendaji wa  nssf  bw. Ramadhani Dau amesema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya ambazo zinaiingizia michango mingi zaidi katuika mfuko huo  ambapo amesema kuwa mwezi huingiza  milioni 432  kwa mwezi.
 Bw.Dau aliongeza kuwa mchango huo kwa mwezi ni mkubwa sana kwa kuwa ndani ya mwaka mzima ni sawa na shilingi biloni tano hali  mbayo inaashiria kuwa kukiwa na ofisi hiyo karibu kutaongeza idadi ya wananchama wengine wapya katika mfuko huo.
 “mfuko wa hifadhi ya jamii umeona ni vyema kama watatumia njia nzuri kuwa karibu na wananchama wake kwa kuweka ofisi hii nyinyi ili kuwapunguzia bughudha ya kufuatilia mafao pamoja na kuweka michango yenu hivyo nadhani hii itawasidia sana”alisema bw.Dau
 Aidha alifafanua kuwa lengo la nssf kufungua ofisi hiyo ni ili kuwa karibu na wananchama ili waweze kuweka michango yao kwa urahisi zaidi na kuwapunguzia gharama za kufuatilia mafao wanachama ambapo ahapo awali walikuwa wanalazimika kufuata huduma zote za mfuko mjini Arusha.
 Kwa upande wake Mkurugenzi wa uendeshaji  bw.Cricentus Magori  alisema kuwa shughuli ambazo zinafanyika katika wilaya hiyo haswa mashamba makubwa ya maua ambayo yapo maeneo mbalimbali,shughuli za uchimbaji wa madini  ndio chachu ya kupata michango mingi ,na wnachama wengi katika  wilaya ya arumeru.
 Bw.Magori alisema kuwa kwa sasa wilaya hiyo ina wanachama elfu saba  ambapo alisema kuwa  wameona ni muhimu kufungua ofisi ili kuwapatia huduma na kuondoa usumbufu wa kufuata huduma hizo mjini Arusha.
 Katika uzinguzi huo uliofana sana ulifanyika katika  kata ya usa river wilayanu arusmeru na kuwashirikisha wafanyakazi na wanachama wa mfuko huo pamoja na wadau mbalimbal

No comments:

Post a Comment