Samsung Senior Manager Bw.  Simon Kirithi akizungumza na waandishi wa habari katika duka la kampuni hiyo lililopo Quality Center jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumzia kuanza kwa Wiki ya Samsung Tanzania 2012 mnamo Oktoba 29 hadi Novemba 3 mwaka huu, na kusema wiki hiyo imelenga kujitolea katika maendeleo ya jamii, burudani na uvumbuzi wa teknolojia, ambapo watumiaji watapata nafasi ya kushiriki na kuona bidhaa na huduma za Samsung kwa vitendo.
Afisa wa Samsunga Ms. Tessa Calleb akikabidhi Aziz Kindamba wa Clouds zawadi ya kopmyuta ndogo ya mkononi baada ya kujishia katika bahati nasibu iliyoendeshwa kwa waandishi wa habari. 
Pichani Juu na Chini ni Afisa wa Samsunga Ms. Tessa Calleb akikabidhi zawadi mbali mbali kwa washindi wa bahati nasibu kwa waandishi wa habari.
Dhamira ya Samsung na imani katika soko la Afrika, inaonekana dhahiri kwa kupitia mikakati ya soko lao na kwa kushiriki kwao wenye miradi ya jamii ambayo imeacha hisia ya kudumu miongoni mwa watu.
Sasa kwa kuonyesha zaidi dhamira za malengo yao, Samsung inaadhimisha Wiki ya Samsung Tanzania kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 3 2012.
 Wakati Samsung inaendelea kupanua uwepo wake Afrika, nia yake si tu kushiriki katika shughuli nyingi za jamii inapofanyia kazi – bali kuwa zaidi kuliko tu kuwepo na pia kuchangia ipasavyo na kuleta mafanikio chanya kwenye jamii ambapo wateja wake huishi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Afrika Mashariki Jong O Lee amesema “Sisi tunaelewa kwamba kuwa na mafanikio katika bara la Afrika si kuingia tu soko la Afrika bali inahitaji tabia ya ujasiriamali nakujitolea kusaidia kujenga soko na miundombinu inayoizunguka “.
”Sisi tunatengeneza bidhaa na programu za kipekee zinazoendana na mahitaji,  rasilimali na hali ya waafrika. Sisi tunatengenezaprogramu za waafrika ambazo zina uwezo na ubunifu wa kipekee unaowajengea watu wake kwa kutoa fursa/nafasi barani. Sisi tunatengeneza huduma zinazowalenga  waafrika na zinazopelekea moja kwa moja ukuaji wao .”
 Sambamba na hili, pamoja na umuhimu wa mafanikio na ushirikiano, pamoja na biashara zao za Afrika na ushirikiano wa sekta ya maendeleo, Samsung Electronics imeandaa Wiki ya Samsung Tanzania – wiki ambayo imelenga kujitolea katika maendeleo ya jamii, burudani na uvumbuzi wa teknolojia – ambapo watumiaji watapata nafasi ya kushiriki na kuona bidhaa na huduma za Samsung kwa vitendo.
Shughuli mbalimbali zimepangwa kwa ajili ya wateja kufurahia safu mbalimbali  za bidhaa za Samsungzinazopatikana kupitia matangazo ya ofa maalum zinazotolewakwenye maduka yote ya Samsung, kutakuwa na burudani ya maonyesho ya barabarani na katika vituo vya mauzo ili kuweza kulete bidhaa karibu na wananchi; pamoja na hayo ukinunua bidhaa za samsung kuna ofa nzuri  zinazo kuwezesha kuingia kwenye droo za bahati nasibu zilizo nzuri na za kusisimua.
 Pamoja na shughuli za kusisimua zilizopangwa kwenye wiki ya samsung za kuzunguka mji wa Dar , siku ya mwisho ya wiki mnamo tarehe 3 Novemba, Jumamosi pale Hoteli ya Golden Tulip Marquee, Toure Drive itakua ni siku ya maonyesho.
Samsung imepanga shughuli mbalimbali kwenye siku ya kuzoea Samsung kwa watumiaji kupata fursa ya kujaribu bidhaa mbalimbali za Samsung katika maonyesho, kutumia faida ya bei maalum inayotolewa, na pia kushiriki katika fani mbalimbali za burudani na shughuli za michezo na maonyesho kadhaa ya wasanii mbalimbali na kuwakaribisha wateja wote watakaohudhuria siku yamaonyesho ya Samsung.
Wiki ya Samsung imepangwa kufungwa rasmikwenye sherehe za vijana za ufukweni mwa bahari paleMbalamwezibeach iliyoko Mikocheni ‘B’ kwa Warioba ambapo kutakuwa na zawadi nyingi za kushindaniwa tarehe hiyo ya Novemba 3-Jumamosi kuanzia saa 11 jioni.
 Mbali na shughuli za maonyesho kwa watumiaji, Samsung pia itasaidia jamii kwa kutoa huduma za bure kwa matengenezo ya bidhaa za Samsung (kama vile notebook,kompyuta , kamera na simu za mkononi) na kuongeza uelewa kuhusu hatari za kutumiavifaa vya teknolojia bandia.
 Leealiendelea kusema; “Hii ni hatua ya kusisimua sana kwa Samsung kama kampuni ambayo hivi karibuni imepanuakiwango chake cha warantii kwa wateja wenye bidhaa zilizo na  (Visual Display), vifaa vyenye teknologia ya IT, Vifaa vya digitali, upigaji Digitali na bidhaa za ufumbuzi za Digital Air.
Wateja sasa kufurahia kiwango cha chini miezi 24 ya warantii kwenye bidhaa zote za Samsung, zilizonunuliwa kutoka 1 Mei 2012, na hakuna malipo ya ziada ya hii Kampeni ya Huduma za matangenezo ya bure inaturuhusu kuendelea kuonyesha dhamira hii.”
   “Samsung inasikiliza soko, inajenga ushirikiano na kweli inadhamiriakwa Afrika na watu wake na Wiki ya Samsung, pamoja na kampeni yetu ya Huduma ya matengenezo bure, hii ni mfano mmoja tu wa jinsi sisi tunavyofanikisha hili,” alihitimisha Lee.