KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 18 October 2012


WASHINDI WA SHINDANO LAMAMA SHUJAA WA CHAKULA 2012 WAPATIKANA

Mshindi wa kwanza wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sista Martha Mwasu kutoka mkoani Dodoma (kushoto) akiwa na zawadi  baada ya kuibuka mshindi  wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula, 2012. Katikati ni mshindi wa pili kutoka mkoani Kagera Bi. Emiliana Eligaesha, kulia ni Naibu Waziri Mawasiliano Sayansi  na Teknolojia Mh. January Makamba.
Washindi watatu bora kwenye mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2012 kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri Mawasiliano Sayansi  na Teknolojia Mh. January Makamba wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi ya mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2012.
Mwakilishi Mkazi waShirika la Kimataifa Oxfam Bi. Monica Gorman akimpongeza mshindi wa kwanza wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Sista Martha Mwasu kutoka mkoani Dodoma wakati  wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi ya mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2012.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano Bw. Imani Kajula akiwapongeza washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2012 wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi ya mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula 2012.
Washiriki wa Mashindano ya Mama wa Shujaa wa Chakula 2012 wakiwa zawadi  walizokabidhiwa na Benki ya NMB baada ya shindano hilo

No comments:

Post a Comment