KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Friday 26 October 2012



Kamanda wa polisi mkoani Arusha kamada Liberatus Sabas akionyesha vipande vya kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu lililopigwa nyumbani kwa  katibu wa BAKWATA mkoa wa Arusha Abdul Kareem Jonjo baadhi ya vongopzi wa ulinzi na usalama mkoa wa arusha wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha walifika  nyumbani na hospitalini jijini Arusha leo ili kona hali ilivyo baada ya tukio la kupigwa kwa bomu hilo(Picha na zote na mahmoud AhmadKatibu wa BAKWATA mkoa wa Arusha Abdul Kareem Jonjo akiwa amelazwa hospitali mara baada ya kushabuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni  bomu
……………………………………………
MNAMO TAREHE 25/10/2012 MUDA WA SAA 6:30 USIKU HUKO KATIKA MTAA WA
KANISANI KATA YA SOKONI ONE ILIYOPO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA, MTU
MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA ABDULKARIMU S/O IDD JONJO (52) KATIBU
WA BAKWATA MKOA WA ARUSHA NA NI MKAZI WA SOKONI ONE ALIJERUHIWA KWA
MLIPUKO KATIKA VIDOLE VYAKE VITATU VYA MKONO WA KULIA PAMOJA NAKIDEVUNI.
TUKIO HILO LILITOKEA CHUMBANI KWAKE KATIKA NYUMBA ALIYOPANGA AMBAYO
INYOMILIKIWA NA JAPHET S/O URIO. TAARIFA ZA AWALI ZINAELEZA KWAMBA,
NDUGU ABDULKARIMU S/O IDD AKIWA USINGIZINI GHAFLA ALISHTUSHWA NA SAUTI
YA KISHINDO KILICHOTOKEA DIRISHANI NA MARA BAADA YA KUAMKA ALIONA KITU
KIKINING’INIA DIRISHANI NA ALIPOKIGUSA GHAFLA ULITOKEA MLIPUKO AMBAO
ULIMJERUHI KATIKA MAENEO YA MWILI WAKE YALIYOTAJWA HAPO JUU.
KUFUATIA TUKIO HILO, ALIOMBA MSAADA KWA MAJIRANI AMBAO WALIMPELEKA
HOSPITALI YA MOUNT MERU KWA AJILI YA MATIBABU AMBAPO MPAKA HIVI SASA
AMELAZWA KATIKA HOSPITALI HIYO NA ANAENDELEA VIZURI.
MARA BAADA YA JESHI LA POLISI KUPATA TAARIFA HIYO BAADHI YA ASKARI
WALIKWENDA KATIKA ENEO LA TUKIO NA KATIKA UCHUNGUZI WA AWALI WALIBAINI
KWAMBA MLIPUKO HUO ULIANZIA NDANI YA CHUMBA HICHO NA KUTOKEA NJE
USAWA WA SAKAFU NA UKUTA, PIA KUMETOKEA UHARIBIFU WA VIOO VYA DIRISHA
MOJA NA VIPANDE VYAKE KUANGUKIA NJE NA PIA MADUMU MAWILI YA LITA 10
YALIYOKUWA NA MAJI YALIPASUKA KWENYE VITAKO VYAKE NA MAJI HAYO
KUTAPAKAA KATIKA CHUMBA HICHO.
MPAKA HIVI SASA HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO
NA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA NA UPELELEZI WA KINA ILI
KUWEZA KUBAINI CHANZO, SABABU ZA KUTOKEA KWA TUKIO HILO NA HATIMAYE
KUWAKAMATA WALE WOTE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO. ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS
TAREHE 25/10/2012.

No comments:

Post a Comment