Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea taarifa ya kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Bw Bernard Mbakileki Wizarani Leo. Kamati hiyo ya watu wanane iliundwa tarehe 27 Agosti 2012 kwa ajili ya kuchunguza utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).Waziri wa Uchukuzi ameiahidi Kamati kuwa kila kipengele walichoshauri kwenye ripoti hiyo kitachukuliwa hatua na Mpaka Disemba mwaka huu Utekelezaji wa Mapendekezo ya ripoti yatakuwa yametekelezwa yote.
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Bernard Mbakileki akionyesha Magazeti mbalimbali kwa Waziri wa Uchukuzi,Watendaji wa taasisi za Wizara Uchukuzi pamoja na waandishi wa habari hawapo pichani yaliyokuwa yakiripoti mambo mbalimbali wakati uchunguzi huo ulipokuwa ukiendelea.
Mwenyekiti wa kamati ya ya uchunguzi wa utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Bw Bernard Mbakileki akisistiza jambo kwa Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi,Taasisi zilizo chini ya Wizara na waandishi wa Habari(hawapo Pichani),wakati wa kukabidhi ripoti waliyoiandika kwa Waziri wa Uchukuzi na kuikabidhi leo. Kulia kwa Mweyekiti wa Kamati hiyo ni  Mhe. Mhandisi. Ramo M. Makani.(Mb) ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari(hawapo Pichani)baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya watu wanane aliyoiunda  kwa ajili ya kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA).Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa mapendekezo yalioandikwa kwenye ripoti hiyo yatafanyiwa kazi na kila aliyehusika na ubadhilifu atachukuliwa hatua.
 
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea ripoti ya Kamati iliyoundwa Kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw Benard Mbakileki,Kushoto kwa Waziri Mwakyembe ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, na Kushoto kwa Naibu Waziri huyo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo.