Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yahana Budeba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya sekta ya Uvuvi, Misitu na Wanyamapori na hatua ya serikali ya kupeleka madaraka ya usimamizi  wa maliasili katika ngazi ya kijiji.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yahana Budeba akifungua mkutano wa wadau kutathmini maendeleo ya  ya Uvuvi, Wanyamapori, Misitu na Mifugo jijini Dar es salaam. Mkutano huo uliowahusisha pia wadau kutoka nchi wafadhiri wa miradi ya maendeleo na wadau kutoka asasi za kiraia unalenga kuimarisha usimamizi wa maliasili na kupeleka madaraka ya usimamizi ngazi za vijiji.
Washiriki wa mkutano wa tathmini ya maendeleo   ya sekta ya  Uvuvi, Wanyamapori, Misitu na Mifugo wakijadili masuala mbalimbali kuhusu usimamizi  endelevu wa maliasili  zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mkutano kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wadau kutoka asasi za kiraia zinazoshughulika na uhifadhi wa mazingira na washirika wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi  wa mkutano huo jijini Dar es salaam.(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).