KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday 16 October 2012


SULTANI QABOOS WA OMAN AMTUNUKU NISHANI YA HESHIMA RAIS DKT.JAKAYA KIKWETE


Watoto  wakitanzania ambao wazazi wao wanaishi na kufanya kazi katika ubalozi wa Tanzania nchini Oman wakimkaribisha kwa maua Rais Dkt.Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Muscat jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya Sultani jijini Muscat jana jioni(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya AL Alam jijini Muscat Oman jana jioni muda mfupi kabla ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake.
Sultani wa Oman,Qaboos bin Said Al Said akimtunuku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nishani ya juu ya heshima, Taifa la Oman wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri ya  AL Alam jijini Muscat Oman.
Sultan Qaboos bin Said Al Said akimpongeza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman jana jioni katika kasri ya AL Alam. Jijini Muscat Oman jana jioni .Rais Kikwete aliwasili nchini Oman jana jioni kwa ziara rasmi ya siku tatu(picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment