Mhe. Balozi Salome sijaona akiwapokea wajumbe waliokuwa wakihudhuria mikutano ya IMF na WB hapa nyumbani kwake kwenye ubalozi wa Tanzani ( Tanzania House) kwa chakula cha jioni alichowaandalia.

Wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mikutano ya IMF na WB Jijini Tokyo- Japan wakiwa katika mwaliko rasmi  wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mhe. Balozi Salome Sijaona katika ubalozi wa Tanzania. Kutoka kulia ni Kamishna wa Bajeti Bi. Monica Mwamunyange, katikati ni Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi.  Mwanaidi Mtanda na wakushoto ni Kamishna wa sera Bw. Bedason Shallanda, wakimsikilisa kwa makini Balozi, hayupo kwenye picha.
Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona akimkaribisha rasmi Waziri wa Fedha pamoja na ujumbe kutoka Tanzania kwa chakula cha usiku. kutoka kulia ni Mhe. William Mgimwa Waziri wa Fedha akifuatiwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omary Yusuph Mzee akifuatiwa na Bw.Selivicius Likwilile Naibu Katibu Mkuu Wizara na Fedha na wengineo ni viongozi waliohudhuria hafla hiyo Jijini Tokyo – Japan.
Wajumbe wa mkutano wa IMF na WB wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona alipokuwa anatoa historia fupi ya ubalozi wa Tanzania.
Wajumbe wa mkutano wa IMF na WB wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona alipokuwa anatoa historia fupi ya ubalozi wa Tanzania.
 Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona akimwelezea Waziri wa fedha Mhe William Mgimwa mambo muhimu ambayo yanapaswa kufanyika katika Balozi zetu.
Afisa wa ubalozi Bi Agnes akiwakaribisha wageni chakula cha usiku hapa ubalozini jijini Tokyo Japan.
Wajumbe kutoka Tanzania wakishiriki chakula cha jioni pamoja na Balozi Mhe. Salome sijaona.
Mhe. William Mgimwa akimshukuru Mhe. Balozi Salome Sijaona pamoja na mme wake Mzee Sijaona aliyekulia kwa Mhe. Balozi Salome Sijaona kwa mwaliko wa chakula cha usiku.
 
Mhe. Balozi Salome Sijaona akimweleza Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma juu ya umuhimu wa Mawasiliano Serikalini.(Picha na Scola Malinga).