Waziri wa Kazi na Ajira , Gaudencia Kabaka  akijibu  swali Bungeni mjini Dodoma leo asubuhi juu ya kuwepo mikakati ya mifuko yahifadhi ya jamii kuwapa wastaafu  mafao yao bila usumbufu.
Wastaafu wameshauriwa kutumia  ofisi za mikoa na kanda kuchukua mafao yao badala ya utaratibu uliozoeleka wa  wa sasa kufuata mafao hayo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka ameliambia Bunge leo wakati akijibu swali la Mbunge wa  Busanda (CCM), Lolesia Jeremiah Bukwimba.
Mbunge wa Busanda , Bukwimba alitaka kujua ni mikakati gani inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na mifuko ya jamiikuhakikisha kuwa wastaafu hao hawaendelei kupata kero kwa kufuata mafao yao Dar es Salaam badala ya sehemu zao za kazi .
Mbunge Bukwimba pia alitaka kujua kwa nini wastaafu hawanufaiki na fedha zao wanazoweka kwenye mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii  kabla yakustaafu kama vile kupata mikopo ya kujenga nyumba na shughulizingine.
Waziri Kabaka alisema kuwa kwa sasa mifuko hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)  wameweka mikakati ya kuanzisha utaratibu mzuri wa kutoa mikopo kwa wafanyakazi  kupitia  SACCOS  zawafanyakazi.
Kabaka alitaja faida nyingine kama kutoa mafao ya afya, gharama za shule na nyingine nyingi zikiwa  baadhi ya  faida wazipatazo wafanyakazi kabla ya kustaafu kwao.
Baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania na wageni wengine,  wakiwa Bungeni  leo asubuhi kufuatilia kikao  mjini Dodoma