Rais anayeondoka madarakani Hu Jintao ameahidi kuwa China itafanya mabadiliko ya kisiasa. Hu Jintao amesema pia kuwa nchi hiyo italifanyia kazi suala la kurekebisha uchumi wake.
Chama tawala nchini China hivi karibuni kilimfukuza madarakani mmoja wa viongozi wake wa ngazi za juu Bo Xilai kutokana na tuhuma za mauwaji na visa vya rushwa. Rais Hu Jintao amesema kuwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka ndani ya chama hicho ni lazima yatolewe adhabu kali.
 Mkutano wa chama hicha cha kikomunisti unaoendelea kwa kipindi cha wiki moja hufanyika kila baada ya miaka mitano na utamalizika kwa kukabidhi madaraka kwa Makamu wa Rais Xi Jinping.
Chama kinalenga kufanya Mageuzi yafatayo:
Mkutano maalum wa chama cha kikomunsiti kufanyika kila baada ya mwongo mmoja
Viongozi wenye zaidi ya miaka 68 watasataafishwa
Viongozi wapya wakuu kutajwa.
Viongozi hao wameamuliwa lakini bado hawajatajwa.
Mirengo ni muhimu kuliko sera na mfumo wa uteuzi haueleweki