“Hali ilikuwa tete lakini baadaye , kila upande ulipunguza jazba katika majadiliano kwasababu haya si matatizo ya kibinafsi , lakini ni matatizo ya nchi” ambayo inapaswa kupatiwa ufumbuzi,  hayo ni maneno ya kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo la waasi wa mashariki ya jamhuri ya Congo Jean -Marie Runiga Lugerero akizungumza na shirika la habari la AFP kwa simu.
Waasi  hao wa M23 wametangaza kuanzisha mazungumzo na rais wa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Joseph Kabila,saa chache baada ya mkutano wa kimkoa kulitaka kundi hilo kusitisha mashambulizi yake mashariki mwa nchi hiyo.
Lugerero, ameonya na kuweka wazi kuwa hatua yoyote ya kuondoa majeshi itakuja pale tu baada ya mazungumzo kati ya kundi hilo la waasi na Kabila. Wapiganaji wa M23 watalinda maeneo yao iwapo majeshi ya Congo yatashambulia.