KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 3 November 2012


Luteni Jenerali Mstaafu  Abdulrahman Shimbo akiingia kwenye gari lake aina ya Toyota landcruiser  alilopewa zawadi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo alilitumikia kwa kipindi cha zaidi ya miaka 41 na kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na  mnadhimu mkuu wa Jeshi. . Sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi hilo Mgulani jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA ANNA NKINDA MAELEZO)
………………………………………
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
 MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamnyange amesema wataendelea kuutambua mchango wa Mnadhimu Mkuu Mstaafu wa jeshi hilo, Luteni Jerenali Abdulrahman Shimbo.
 Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na Mwamnyange wakati wa sherehe ya kumwuaga Mnadhimu huyo iliyofanyika katika kambi ya jeshi ya Mgulani jijini Dares Salaam.
 “Ni kiongozi ambaye ametoa mchango wake mkubwa tangu alipokuwa askari hadi Afisa wa ngazi za juu,” alisema Mwanyange.
  Mwamnyange aliongeza kuwa Shimbo, ambaye ametumikia jeshi hilo kwa kipindi cha takriban  zaidi ya miaka 41 alikuwa ni mchakapazi wa hali ya juu, mwadilifu na mwenye nidhamu.
 Akizungumzia kuhusu utendaji wake wa kazi, Shimbo alisema ni kitu cha kujivunia kwani nchi imeendelea kuwa na amani na usalama.
 Aliongeza kuwa alijithidi kudumisha nidhamu na kuwafanya wanajeshi kuwa karibu na wananchi na kuwa wazalendo na upendo kwa nchi yao.
 Shimbo alisema miongoni mwa changamoto ni kushindwa kutekeleza majukumu ya jeshi kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
 Mnadhimu huyo aliagwa rasmi kwa gawaride maalum na kusindikizwa la gari kutoka uwanja wa kambi hiyo hadi geti kuu ambalo lilisukumwa na  maofisa wenye vyeo vya Meja Jenerali.
 Katika sherehe hizo Mwamnyange alimkabidhi funguo wa gari aina ya Landcruser ikiwa ni zawadi ya utumishi wake.

No comments:

Post a Comment