KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 3 November 2012


JK Azindua Taasisi Sayansi Na Teknolojia Ya Chuo Kikuu Cha Nelson Mandela Arusha

 
 
Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kuweka jiwe la Msingi ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 2, 2012. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Mohammed Gharib Bilal. Kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha , Novemba 2, 2012. Kulia ni Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

 
 Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 2, 2012. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dk. DMohammed Gharib Bilal. Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.
  
 Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha.
                       
                                     Picha na OMR

No comments:

Post a Comment