KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday 26 November 2012


BENKI YA NMB YACHANGIA MILIONI 30 KUFANIKISHA UZINDUZI WA MKOA WA KATAVI



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 15  kutoka kwa Robert Pascal Mkuu wa Kitengo cha Kilimo benki ya NMB, kama mchango wa benki hiyo kwa ajili ya kununulia madawati ya shule za msingi  katika mkoa huo, Ikiwa ni  mchango wa benki hiyo katika maendeleo ya elimu Mkoani Katavi, Mkoa wa Katavi umezinduliwa leo na Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda, na kuhudhuriwa na wananchi wengi wa mkoa hou.
Mbali na fedha hizo benki ya NMB pia imetoa kiasi cha shilingi milioni 15 zingine na vifaa vya michezo ikiwemo mipira na jezi kwa ajili ya timu za mpira wa miguu za mkoa wa Rukwa na Katavi kwa ajili ya kufanikisha mchezo wa mpira wa miguu kati ya timu hizo wakati wa uzinduzi  katika  mkoa huo , pamoja na  maandalizi mengine ya shughuli za uzinduzi, jumla ya fedha iliyotolewa na Benki ya  NMB ni  shilingi milioni 30 za Kitanzania.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal (kushoto)akiteta jambo na Wziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mizengo Pinda, wakati wa Kongamano la kutathmini mrejesho wa kongamano la Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Lake Tanganyika uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana mjini Mpanda.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe akikaribisha wageni mbalimbali waliofika kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano hilo na Mkoa wa Katavi lililofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Maji Mjini Mpanda juzi na kumalizika jana.

Waziri Mkuu wa Mizengo Pinda akimshukuru mama Domina Ferouz Mkuu wa Biashara kati ya benki ya NMB na Serikali, mara baada ya kupokea hundi hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa mkoa wa Katavi, katikati ni Lucrencia Makinya Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini NMB.
Wananchi wakitembelea moja ya Banda ya wawekezaji wa kigeni wakati wa maonyesho hayo katika maonyesho wakati wa uzinduzi wa mkoa wa Katavi uliofanyika leo mjini Mpanda.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Paza Mwamlima akitoa utaratibu wakati wa Kongamano la Tathmini ya Mkutano wa Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika lililofanyika sambamba na uzinduzi wa mkoa wa Katavi kuanzia juzi na kumalizika  jana mjini Mpanda huku uzinduzi wa mkoa huo ukifanyika leo.
Baadhi ya maofisa  mbalimbali wa Serikali waliohudhuria katika Kongamano hilo lililofanyika mjini Mpanda mkoa mpya wa Katavi.
Mabalozi kutoka nchi mbalimbali walihudhuria kongamano hilo zikiwemo Burundi, Misri Zambia, Japan na DRC Congo hapa wakifuatilia Mada katika  kongamano hilo.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akikaribishwa na Lucrencia Makinya Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini Benki ya NMB, katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki ya NMB kwa ajili ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kwenye hoteli ya Lyamba lya Mfipa mjini Mpanda
Wafanyakazi wa benki ya NMB wakijumuika katika picha ya pamoja mara baada ya kula Chakula cha jioni na wakuu wa Mikoa na  wilaya  kwenye hoteli ya Lyamba Lya Mfipa mjini Mpanda.
Maofisa mbalimbali wa benki ya NMB  kutoka makao makuu , Mbeya  na Mpanda wakiwa katika picha ya pamoja wakati benki hiyo ilipoandaa chakula cha jioni kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye hoteli ya Lyamba Lya Mfipa mjini Mpanda jana
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza  na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika maonyesho yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi mjini Mpanda.

No comments:

Post a Comment