KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 3 November 2012


MAMLAKA YA UDHIBITI WA MIFUKO YA JAMII (SSRA) YATOA SEMINA KUHUSU SEKTA YA HIFADHI YA JAMII KWA WABUNGE, BUNGENI DODOMA LEO


Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii Bi. Irene Isaka (Hayupo Pichani) alipokuwa akiwasilisha maada kwa Waheshimiwa Wabunge kuhusu Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi Mhe. Andrew Chenge pamoja na Waziri wa Kazi na ajira Mhe. Gaudensia Kabaka
PICHA NA OWEN MWANDUMBYA WA BUNGE
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii Bi. Irene Isaka akiwasilisha maada kwa Waheshimiwa Wabunge kuhusu Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dkt. Emmanuel Humba akitoa maelezo kuhusu huduma za Mfuko Taifa wa Bima ya Afya kwa Waheshimiwa Wabunge katika Ukumbi wa Pius Msekwa Dodoma 
Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Agrey Mlimuka akiwasilisha mada kuhusu huduma za Hifadhi ya Jamii Nchini kwa Waheshimiwa Wabunge
Katibu Mkuu wa TUCTA Ndg. Hezron Kaaya akitoa mada kwa Wabunge kuhusu Mtizamo wa Hifadhi ya Jamii kwa upande wa Wafanyakazi
Wadau kutoka Mifuko ya Jamii wakifuatilia mada hizo
Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii Bi. Sara Msika akishiriki semina hiyo 
Waheshimiwa wabunge wakifuatilia mada katika semina hiyo 
Waheshimiwa wabunge wakifuatilia mada katika semina hiyo 

No comments:

Post a Comment