KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 3 November 2012


LUTENI JENERALI SHIMBO AAGWA RASMI LEO BAADA YA KUSTAAFU


Askari wa kikosi cha bendera kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima  kwa mwendo wa haraka mbele ya Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (hayupo pichani) wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya jeshi hilo Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu  Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 na kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na  mnadhimu mkuu wa Jeshi.
PICHA NA ANNA NKINDA WA MAELEZO
Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakitoa heshima  kwa mwendo wa pole  mbele ya Luteni Jenerali Mstaafu A Shimbo (hayupo pichani) wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu  Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41  kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na  mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Luteni Jenerali Mstaafu  Abdulrahman Shimbo (kushoto) akiangalia kwa furaha funguo za gari aina ya Toyota landcruiser  alilopewa zawadi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo alilitumikia kwa kipindi cha zaidi ya miaka 41 huku Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange akimuangalia. Sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi hilo Mgulani jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meja Generali Grace Mwakipunda
Luteni Jenerali Mstaafu  Abdulrahman Shimbo (aliyesimama kwenye gari)  akisindikizwa  maafisa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiwa ni kuhitimisha  sherehe za kumuaga rasmi zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu  Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41  kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na  mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Baadhi ya  askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiangalia gwaride  la sherehe za kumuaga Luteni Jenerali Mstaafu  Abdulrahman Shimbo (hayupo pichani) zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam.
Ndugu, jamaa na marafiki wa Luteni Jenerali Mstaafu  Abdulrahman Shimbo (wan ne mstari wa mbele kulia)  wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa   sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam.Wa katikati mstari wa mbele ni  Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange.
Luteni Jenerali Mstaafu  Abdulrahman Shimbo akikagua kikosi cha askari wa kike kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa   sherehe za kumuaga rasmi zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu  Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41  kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na  mnadhimu mkuu wa Jeshi.

No comments:

Post a Comment