KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 4 October 2012


KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA DAR ES SALAAM CHAFANYIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam leo. Pamoja na mambo mengine amewataka watendaji wa Halmashauri na Manispaa za jiji la Dar es salaam kusimamia kikamilifu matumizi sahihi ya barabara ili kuondoa tatizo la msongamano wa magari jijini Dar es salaam. Wengine wanaoonekana ni Mhe. Idd Azzan(Mb) Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es salaam na Michael Mungaya kaimu (kulia) Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam.
Wajumbe wa kikao hicho wakiwemo wakiwemo wabunge wa Dar es salaam Halima Mdee (CHADEMA) jimbo la Kawe (wa kwanza kushoto nyuma) na Abbas Mtemvu Mbunge wa jimbo la Temeke (CCM), wa pili kutoka kushoto mstari wa nyuma wakifuatilia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi na maazimio ya vikao mbalimbali vilivyofanyika.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kikao cha Bodi ya barabara kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili manispaa ya Kinondoni ikiwemo baadhi ya watu waliojenga maeneo yasiyoruhusiwa kutumia vibaya uhuru wa mahakama kufungua kesi na kukwamisha uendelezaji wa baadhi ya miradi ya barabara na ubomoaji wa baadhi ya nyumba zilizojengwa kinyumme cha utaratibu jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya  Temeke Bi. Magreth Nyalile akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki wa kikao hicho wakiwemo wabunge kuhusu hatua zinazochukuliwa na Halmashauri ya Temeke kujenga miundombinu na maegesho yatakayotumiwa  na malori yanayotoka bandarini na kupunguza  kero kwa watumiaji wengine wa barabara hizo kutokana na kushindwa kupitika kutokana na msongamano wa malori hayo.
Washiriki wa kikao cha Bodi ya Barabara ya mkoa wa Dar es salaam wakiwemo wakurugenzi wa Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa kikao hicho leo jijini Dar es salaam.(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).

No comments:

Post a Comment