KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday, 15 October 2012


Dkt. BILAL AWAAGA MAHUJAJI


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka. Makamu alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni Oktoba 14, 2012 na kuzungumza na Mahujaj hao kuwaaga na kuwakabidhi  Misahafu kila mmoja kabla ya kuondoka.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi  Misahafu, mmoja kati ya Mahujaj 150, wakati alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, 2012 kwa ajili ya kuwaaga Mahujaj hao walioondoka kuelekea Saud Arabia  mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka
  Sehemu ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment