Mkurugenzi wa Maisha Plus,Masoud Kipanya (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB ,Imani Kajula (pili kulia) ,Mwakilishi wa Idara ya Kilimo wa NMB, Carol Nyangaro (wa pili kushoto) na Meneja wa Mikopo Midogo ya Biashara, Mashaga Changarawe.
………………………………………………
NMB ikiwa wadhamini wakuu wa mpango wa mama shujaaa wa chakula, imewatembelea washiriki wa mama shujaa wa chakula katika kijiji i cha Maisha Plus na kuwapa elimu ya kifedha kupitia mpango wa NMB Financial Fitness.
NMB kupitia mpango wa NMB Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha imepata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine mengi.
Vilevile, Washiriki hao walielimishwa kuhusu Mikopo Midogo na kati ya kibiashara pamoja na mikopo ya kilimo.
NMB inaamini udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB,Imani Kajula (kulia) akiwagawia jarida la NMB Financial Fitness baadhi ya wakinamama wa Mama Shujaa wa Chakula katika kambi ya Maisha Plus, jarida hilo lina maelezo mengi yanayohusu uelewa wa matumizi ya fedha.
No comments:
Post a Comment