WAKAZI WA DAR WAFURAHIA USAFIRI WA GARI MOSHI.
Bi. Rose Ngauga akizungumza na mwandishi wetu aliyemtembea ofisini kwake kujua mawili matatu kuhusiana na usafiri huo.
WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wamefurahia kuanza kwa usafiri wa treni waliousubiri kwa muda mrefu ulioanza hivi karibuni.
Abiria wakigombea kupanda treni kutoka katikati ya jiji kuelekea Ubungo.
Kamera yetu leo ilitua katika ofisi ya mkuu wa kituo kinachodili na usafiri huo, Bi. Rose Ngauga na kuzungumza mambo kadhaa kuhusiana na usafiri huo.
Ngauga alisema kuwa usafiri huo siyo nguvu ya soda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na kwamba utakuwa endelevu.
Wanafunzi wakipanda katika behewa lao maalumu tayari kwa safari.
Bi. Rose akimuonyesha mwandishi wetu (hayupo pichani) tiketi zinazotumika kwa abiria wa kawaida na wanafunzi.
Abiria wakiwa katika dirisha la kukatia tiketi.
Wanafunzi wakikata tiketi katika dirisha maalumu kwa ajili yao.
Kichwa cha treni kikiunganishwa na mabehewa kabla ya kuanza safari.
Abiria wakiwa wameketi ndani ya behewa wakisubiri kuanza safari.
Mkuu wa Kituo cha Reli, Bi. Rose Ngauga akikagua mabehewa kabla ya gari moshi kuanza safari jana saa 9.40 alasiri.
…akikabidhiwa ripoti.
Gari moshi likiwa katika mwendo na baadhi ya abiria wakionekana wakichati na simu.
Mwandishi mwanadamizi wa Global Publisher, Haruni Sanchawa akishuka kutoka katika treni hiyo maeneo ya Ubungo Maziwa ambako treni hiyo umalizia safari yake.
Abiria wakishuka kwenye treni.
Pamoja na usafiri huo kuanza, mafundi wa shirika la reli bado wanaendelea na ukarabati wa reli kama wanavyoonekana pichani.
(HABARI PICHA : Haruni Sanchawa / GPL)
No comments:
Post a Comment