MZEE WA MIAKA 50 ANUSURIKA KUUAWA KWA KUTAKA KUIBA MBAO MKOANI SINGIDA.
Mwanaume anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 50 aliyenusurika kuuawa kwa kile kilichodaiwa alikuwa akitaka kuiba mbao kwenye nyumba moja mtaa wa Misuna mjini Singida.Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina moja la Mwera (pichani) ambaye anafanya kazi ya kusukuma toroli stand mpya ya Misuna,inadaiwa usiku wa kuamukia leo wakati akijaribu kuingia ndani ya nyumba ambayo ipo kwenye hatua za mwisho mwisho kukamilika kupitia dirishani, miguu yake ilinasa kwenye nondo za dirisha na kushindwa kuingia ndani.
Baada ya kushindwa kuingia ndani,wakati akitaka kutoa kwa nguvu miguu yake iliyonasa kwenye nondo,mikono yake iliteleza na kusababisha aning’ing’e kichwa chini na miguu ikiwa juu dirishani kuanzia alfajiri hadi aliponasuliwa saa mbili kasoro robo asubuhi.
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida wakimshangaa mwanaume huyo huku akijaribu kuficha uso wake.Alinusurika kuuawa baada ya mpiga debe mmoja Sele,kuwasihi watu hao ambao tayari walikuwa wamebeba silaha za jadi.Picha ya pili,baada ya mpiga picha hii kumvua fulana yake kwa nguvu na sura yake kuonekena.Picha na Nathaniel Limu.
No comments:
Post a Comment